RAIS MAGUFULI : UTUMBUAJI UTAENDELEA 2020 - 2025Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amesema utumbuaji kwa watumishi wa umma wazembe, wala rushwa, wezi na wabadhirifu, utaendelea katika miaka mitano ijayo. 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo kwenye Uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema, watumishi wezi, wabadhirifu bado wapo hivyo ataendelea kuwang’oa.

“Watumishi wazembe, wala rushwa, wezi, wala mali bado wapo. Miaka mitano ijayo tutawashughulikia, kwa kifupi niseme utumbuaji utaendelea,” amesema Rais Magufuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post