Wahamiaji Haramu 6 Wakamatwa Njombe

 Wahamiaji haramu 6 waliokuwa wameweka kambi katika Makaburi ya Kipagamo Nje kidogo ya mji wa Makambako wamekamatwa na kikosi cha uhamiaji mkoani Njombe wakitokea nchini Ethiopia .

Mbali na kuwatia nguvuni wahamiaji hao , kikosi hicho pia kinawashikilia watanzania 2 kwa tuhuma za kuhusika biashara haramu ya usafirishaji wa raia wa kigeni kinyume cha taratibu pamoja na gari ndogo aina ya Rava 4 ambayo inadaiwa kutumika kuvusha watu hao.

Akizungumzia kukamatwa waethiopia hao afisa uhamiaji mkoa wa Njombe John Yindi amesema watu hao wameingia nchini wapitia Horogoro wakisaidiwa na watanzania waliokosa uzalendo na kudai kwamba tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi yao.

Kamishna Yindi amesema hakuna upenyo kwa wahamiaji haramu katika mkoa wa Njombe kwa kuwa jeshi limejidhatiti katika vizuizi vyote kikiwemo cha Ziwa Nyasa kilichopo wilayani Ludewa.

Kwa Upande wake Daniel Shoo mkaguzi msaidizi wa kituo kidogo cha Uhamiaji mjini Makambako anasema doria za usiku na mchana katika mji huo zimekipa mafanikio makubwa kikosi cha uahamiaji na kutoa rai kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo viovu ikiwemo kuingiza wahamiaji nchini kinyemela.

Shoo amesema katika kizuizi cha Makambako wamekuwa wakikamata wahamiaji haramu wengi wakitokea nchi jirani jambo ambalo linawafanya kuwa macho muda wote huku akiwataka wananchi kuwaripoti watu wanaowatilia shaka endapo watawabaini katika maeneo yao.


Amesema kuendelea kufanya biashara haramu ya kuingiza wageni kinyemela nchini kuna hatarisha usalama wa taifa kwasababu wanaweza kutumika kufanya maovu nchini.


Kwa uchunguzi wa awali unaonyesha wameingia kupitia Mombasa wakitegemea kuingia Africa kusini kutafuta maisha.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments