G20 YAREFUSHA MUDA WA MATAIFA MASIKINI KULIPA MADENI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, October 15, 2020

G20 YAREFUSHA MUDA WA MATAIFA MASIKINI KULIPA MADENI

  Malunde       Thursday, October 15, 2020


Mataifa ya kundi la G20 yamekubaliana kurefusha kwa miezi sita muda wa kulipa madeni kwa mataifa maskini yaliyoathiriwa na janga la virusi vya corona .

Wakati wa mkutano uliofanyika kwa njia ya video, mawaziri wa fedha na magavana wa kundi la G20 wameridhia kusogeza mbele hadi Juni 2021 muda wa mwisho kwa mataifa masikini kuanza tena kulipa madeni yake ili kuzisaidia nchi hizo kupambana na janga la COVID-19.

Usimamishaji wa kulipa madeni ulikuwa unafikia tamati mnamo mwezi Novemba mwaka huu na kundi la G20 limesema muda wa nyongeza uliokubaliwa jana unaweza kurefushwa tena wakati wa majadiliano yatakayofanyika wakati wa majira ya kiangazi mwaka 2021.

Waziri wa fedha wa Saudi Arabia Mohammed al-Jadaan aliyekuwa mwenyeji wa mkutano hwa G20 amesema ingawa uchumi wa dunia unaimarika taratibu, mataifa masikini bado yanakabiliwa na hali mbaya kutokana na athari za janga la COVID-19Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post