ATUPWA JELA MIAKA 7 KWA KUTUMIA JINA LA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, October 3, 2020

ATUPWA JELA MIAKA 7 KWA KUTUMIA JINA LA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

  Malunde       Saturday, October 3, 2020

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Issa Mohhamed (27) miaka saba jela katika makosa 11 ikiwemo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kujitambulisha na kutumia jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Hukumu hiyo imetolewa jana Oktoba 2,2020 na Hakimu Mkazi Augustina Mmbando ambapo upande wa mashtaka umethibisha kwamba mshitakiwa alitenda makosa hayo.

Katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Nicholaus Joseph,Hamis Tembo na Wakati Mwichande ambao hawakukutwa na hatia yoyote.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inadaiwa Kati ya Machi 10 na 17,2016 ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, mshtakiwa alijitambulisha kama Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambapo pia alighushi barua ikionesha imetoka ofisi ya Waziri Mkuu kwenda kwa makampuni tofauti ikiwataka kutoa Milioni 25 za Kitanzania kama punguzo la kodi.

Aidha mshtakiwa huyo baada ya kupata dhamana alitoroka hivyo anatafutwa kwa ajili ya kutumikia adhabu hiyo.
 Chanzo - EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post