ROSE MUHANDO AIBUKIA KWENYE MKUTANO WA MAGUFULI SONGWE



Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli upande wa kulia, kushoto ni msanii Rose Muhando

Kwa mara ya kwanza baada ya ukimya wa muda mrefu bila kuonekana kwenye shughuli za sanaa, msanii maarufu wa Injili hapa nchini Tanzania Rose Muhando ameibukia kwenye mkutano wa kampeni za mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli.

Mkutano huo wa hadhara umefanyika Vwawa Mjini katika Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, ambapo Dkt Magufuli alimpatia zawadi ya kofia kama alivyowafanyia wasanii wengine kama Alikiba, Harmonize, Kala Jeremiah, Linex na wengineo.

"Asante Mungu wangu wa mbinguni, asante Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JPM" ameandika Rose Muhando 

Kimuonekano na nguvu ambayo aliionesha wakati anaimba kwenye jukwaa imewatoa hofu mashabiki zake ambao walidhani kama bado Rose Muhando anasumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Ikumbukwe tu kipindi cha nyuma Rose Muhando alikuwa ana matatizo ya kiafya ambayo yalisababisha watu kuongea mengi kuhusu yeye hadi kufikia hatua ya kwenda kuombewa kwa wachungaji wa Kenya pia kuna muda alionekana akipatiwa maombi kwenye Kanisa la Mlima wa moto chini ya marehemu Bi Gertrude Rwakatare.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527