Picha : BENKI YA CRDB YAHITIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUNYWA CHAI NA WAFANYAKAZI WA MAKAMPUNI YA GAKI


Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja akimkabidhi zawadi Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB imehitimisha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na East African Spirits (T) Ltd vinavyomilikiwa na Mwekezaji Mzawa Gaspar Kileo ambaye amekuwa mteja mkubwa wa Benki hiyo kwa takribani miaka 32.

Akizungumza wakati wa kunywa chai hiyo ya pamoja leo Ijumaa Oktoba 16,2020 katika viwanja vya Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd vilivyopo Ibadakuli Mjini Shinyanga,Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja amesema lengo la chai hiyo ni kuwashukuru wateja wao hao wakubwa.

“Benki ya CRDB inasherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo mwaka huu tulipanga kusherehekia kwa muda wiki mbili.Leo tumefika hapa kwa ajili ya kufunga Wiki ya Huduma kwa wateja hapa katika eneo lenu la kazi ili kuwashukuru kwa kuwa wateja wetu wakubwa”,amesema Segeja.

“Viwanda hivi vimechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa Benki ya CRDB ndiyo maana nasi tumeona umuhimu wa kufika hapa ili kusherehekea nanyi wiki ya huduma kwa wateja kwa kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa viwanda hivi”,ameeleza Segeja.

Segeja amewaomba wafanyakazi wa Kampuni hizo kuendeleza  mahusiano na ushirikiano wao kwa Benki ya CRDB huku akibainisha kuwa Benki hiyo inaendelea kupokea maoni ya wateja ili kuboresha huduma za kibenki.

Kwa upande wake, Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice ameishukuru Benki ya CRDB kuandaa chai ya pamoja na wafanyakazi wake.

Kileo maarufu kwa jina la Gaki  ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) ameahidi kuendelea kushirikiana na Benki ya CRDB ambayo wamekuwa wakiitumia kupitishia mishahara ya wafanyakazi wake kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Wakati wa kunywa chai hiyo, Gaki akiwa amevaa Aproni aliongoza zoezi la kuhudumia/kugawa chai kwa wafanyakazi wake ambayo iliandaliwa na benki ya CRDB akisaidiana na viongozi wa Benki ya CRDB akiwemo Beatus Segeja kutoka CRDB Makao makuu, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui, Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney na Meneja Biashara Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Katikati ni Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice akizungumza na viongozi wa Benki ya CRDB baada ya kuwasili katika kiwanda cha Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd kwa ajili ya kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa viwanda vya Gaki leo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui. Wa kwaza kulia ni Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo (wa pili kulia) akiwa na Viongozi wa Benki ya CRDB katika viwanja vya Kampuni ya East African Spirits (T) Ltd) kabla ya kuanza kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja akieleza lengo la Benki ya CRDB kuandaa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni za GAKI.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja akiyashukuru Makampuni ya GAKI kwa kuendelea wateja wa Benki ya CRDB
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja akiwaomba wafanyakazi wa Benki ya CRDB kuendelea kuwa wateja wazuri wa Benki ya CRDB
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja akimkabidhi zawadi Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice. 
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja akimkabidhi zawadi Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice. 
 Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice akionesha zawadi aliyopewa na Benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akizungumza na wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI kabla ya kuanza kunywa nao chai ya pamoja ambapo aliwashukuru kwa kuendelea kuitumia na kuiamini Benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akizungumza kabla ya kuanza kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akimtambulisha Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamis Iddi (kulia).
Gaspar Kileo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd kinachojihusisha na uchambuzi wa pamba, Gaki Transport Ltd inayohusika na usafirishaji wa mizigo na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd inayozalisha vinywaji maarufu Diamond Rock, Hanson’s Choice akiishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni yake ya GAKI.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo akizungumza kabla ya kuanza kunywa chai iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wafanyakazi wa makampuni ya GAKI.
Mkurugenzi Msaidizi wa Makampuni ya GAKI, Humprey Kileo akitoa neno la shukrani kwa Benki ya CRDB
Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo akiwa amevaa Aproni na viongozi wa Benki ya CRDB na Makampuni ya Gaki akitoa utaratibu wa kuhudumia/kugawa chai kwa wafanyakazi wake kuwa yeye ndiyo ataongoza zoezi kwa kuwahudumia wafanyakazi wake.
Wafanyakazi wa Level One Pub ya Mjini Shinyanga wakiwa wamevaa Aproni tayari kabisa kwa kujiandaa kugawa chai kwa wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki. Hata hivyo zoezi la kuhudumia wafanyakazi wa makampuni hayo likifanywa na Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo, viongozi wa Makampuni ya Gaki na Viongozi wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo viongozi wa Benki ya CRDB na Makampuni ya Gaki wakiwa wameshikilia vitafunwa wakati wa zoezi la kunywa chai ya pamoja
Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo viongozi wa Benki ya CRDB na Makampuni ya Gaki wakiwa wameshikilia vitafunwa wakati wa zoezi la kunywa chai ya pamoja
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd , Gaspar Kileo (akiwahudumia chai) akigawa chai kwa wafanyakazi wake. Chai hiyo imeandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd , Gaspar Kileo (akiwahudumia chai) akigawa chai kwa wafanyakazi wake. Chai hiyo imeandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd , Gaspar Kileo (akimhudumia chai) akigawa chai kwa mfanyakazi wake. Chai hiyo imeandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd , Gaspar Kileo na Mkurugenzi Msaidizi wa Makampuni hayo , Humphrey Kileo  ( wa kwanza kushoto) wakigawa chai kwa wafanyakazi wao. Chai hiyo imeandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Wafanyakazi wa Makampuni Gaki wakiendelea kupata huduma ya chai
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd, Gaki Transport Ltd na Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits (T) Ltd , Gaspar Kileo (akiwahudumia chai) akigawa chai kwa wafanyakazi wake. Chai hiyo imeandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja na Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo wakiendelea kugawa vitafunwa/chai kwa wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja ( wa kushoto)  wakiendelea kugawa vitafunwa/chai kwa wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja wakiendelea kugawa vitafunwa/chai kwa wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo akigawa chai kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo akigawa chai kwa Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja, kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo akigawa chai kwa Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamis Iddi
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akiwa amembebea chai (akimhudumia) mfanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akiwahudumia chai wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akizungumza jambo wa akihudumia chai wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akiwashukuru wageni wa Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo akiwemo Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, kupitia CCM, Patrobas Katambi wa nne kushoto.
Viongozi wa Makampuni ya GAKI wakiteta jambo wakati wakimhudumia chai mfanyakazi wa makampuni hayo.
Wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI wakiendelea kunywa chai iliyoandaliwa na Benki ya CRDB
Wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI wakiendelea kunywa chai iliyoandaliwa na Benki ya CRDB
Mkurugenzi wa Makampuni ya GAKI, Gaspar Kileo akinywa chai na Viongozi wa Benki ya CRDB baada ya kumaliza kugawa chai.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali za Benki na Miundombinu ya Uendeshaji Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Beatus Segeja (katikati), Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney wakinywa chai baada ya kumaliza kuwahudumia wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki.
Wafanyakazi wa makampuni ya Gaki wakinywa chai
Zoezi la kunywa chai likiendelea
Wafanyakazi wa makampuni ya Gaki wakiendelea kunywa chai
Wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki wakichukua Juisi
Mfanyakazi wa Kampuni ya Gaki Transport Ltd, Titto Bundala akitoa neno la shukrani kwa Benki ya CRDB kwa niaba ya wafanyakazi wenzake.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye viwanja vya Makampuni ya GAKI
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akizungumza baada ya zoezi la kunywa chai ya pamoja na wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI na kuwaomba kuendelea kushirikiana na Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Gaki, Gaspar Kileo akiishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa chai kwa ajili ya wafanyakazi wa makampuni yake.
Wafanyakazi wa Makampuni ya GAKI wakiendelea kunywa chai iliyoandaliwa na Benki ya CRDB akitoa neno la shukrani kwa uongozi na wafanyakazi wa Makampuni ya Gaki baada ya kunywa chai ya pamoja.
Viongozi wa Benki ya CRDB wakipiga picha pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Ltd baada ya kumaliza kunywa chai
Viongozi wa Benki ya CRDB wakipiga picha pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Gaki Transport Ltd baada ya kumaliza kunywa chai
Viongozi wa Benki ya CRDB wakipiga picha pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Gaki Investment Ltd baada ya kumaliza kunywa chai

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments