TUNDU LISSU LEO ATAZINDUA KAMPENI KANDA YA KUSINI KATIKA UWANJA WA SABASABA, MJINI MTWARA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, September 6, 2020

TUNDU LISSU LEO ATAZINDUA KAMPENI KANDA YA KUSINI KATIKA UWANJA WA SABASABA, MJINI MTWARA

  Malunde       Sunday, September 6, 2020

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA  Tundu  Lissu leo Septemba 6, 2020. atazindua kampeni Kanda ya Kusini (Lindi, Mtwara na Ruvuma) katika Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara.


Jana alikuwa Kanda ya Nyasa, katika viwanja vya Nzovwe, jijini Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine aliahidi kujenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za Machinga na Mamalishe  ambayo yatakuwa wazi usiku na mchana. 


Lissu alisema baadhi ya wananchi huwa wanachelewa kufika kwenye miji yao wanapokuwa wametoka safarini na hivyo kukosa huduma za kununua mahitaji kwenye masoko kutokana na masoko hayo kufungwa .“Tutajenga masoko maalum kwa kushirikiana na sekta binafsi kwenye maeneo mbalimbali ili machinga wetu wafanye biashara hapo kwa uhuru na kila mmoja atakuwa na chumba chake,” aliahidi.

Vilevile, Lissu alisema serikali yao itajenga majengo maalumu kwenye maeneo ya stendi za mabasi kwa ajili wa wauzaji vyakula, maarufu mamalishe na babalishe, ili wafanyie biashara zao huko kwa uhuru.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post