TAASISI YA SHAMSUL MAARIFA ISLAMIYYAH YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA MKOA WA TANGA BOMBO


Mudiri wa Taasisi ya Shamsul Maarifa Islamiyyah Shehe Samiri Hemed kulia akipimwa kabla ya kuanza zoezi la uchangiaji wa damu kwa ajili ya kuongeza damu kwenye benki ya damu salama katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.
 ***

TAASISI ya Shamsul Maarifa Islamiyyah ya Jijini Tanga imeendesha zoezi la utoaji na uchangiaji wa damu kwa ajili ya kuongeza damu kwenye benki ya damu salama katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.


Uchangiaji huo ulifanyika kwenye taasisi hiyo ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Taasisi hiyo tokea ilipoanzishwa miaka 20 iliyopita ambayo hufanyika kila mwaka ikiwamo ufunguzi wa madarasa mapya.


Akizingumza na waandishi wa habari Mudiri wa Taasisi ya Shamsul Maarifa Islamiyyah Shehe Samiri Hemed alisema huo ni mwaka wa 20 tokea walivyoanza madrasa hiyo mwaka 2000.


Alisema kwamba wapo kwenye kumbukumbu yao ya kila mwaka kusherekea kuadhimisha elimu na miaka 20 ya Shamsi Maarifa ambapo wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali wa kijamii.


Shehe Samir alisema moja ya shughuli ambayo wanaifanya kuelekea maadhimisho hayo ni zoezi la utoaji na uchangiaji wa damu kwa ajili ya kuongeza damu kwenye benki ya damu.


Alisema hilo ni moja ya mafunzo ya waislamu kusaidiana na kumsaidia mwengine akiwa kwenye hali ya uzima na ugonjwa kama wanavyofahamu damu kuwepo kwenye benki ya damu ni moja katikati vitu muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya afya ya wanadamu kuisaidia jamii.


“Kwani mtu anaweza kwenda hospitali kwa hali ya sasa hata akienda na mchangiaji wa damu wa kumtolea kama benki ya damu hakuna kitu damu hiyo hawezi kuongezewa mgonjwa hivyo tupo kuisaidia jamii tunafanya zoezi hilo mara kwa mara kuchangia damu inapohitajika”,alisema.

 Aidha alisema safari hii wameifanya iwe rasmi kusherehekea miaka 2o ya shamsi maarifa itakayokwenda samabamba na ufunguzi wa madarasa mapya 10 waliyoyapata kupitia ufadhili wa Taasisi inayoitwa Fildaus.

Hata hivyo alisema majengo hayo yatatumika kusomea hivyo watashiriki kufanya ufunguzi wa madarasa hayo na wamealika wageni kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi ambao watashiriki kwenye maadhimoisho hao ya kuadhimisha miaka 20.


Awali akizungumza katika halfa hiyo Naibu Katibu Mkuu wa Shamsul Maarifa Islamiyyah Hamisi Haruna Mbolele alitoa wito kwa jamii kushirikiana na Taasisi ya Jai katika masuala hayo huku akiziomba taasisi nyengine ikiwemo Shamsul, Zaharau na Maawal waweze kujumuika kwenye jambo hilo.


Alisema kilele cha maadhimisho ya Taasisi hiyo kitafanyika Jumapili wiki hii huku kwa siku zinazoendelea itaanza Septemba 4 huku akiendelea kutoa wito kwa taasisi nyengine ambazo zinaweza kujitokeza kuchangia damu na watu mbalimbali wafike.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527