MAALIM SEIF AAHIDI KUIFANYA ZANZIBAR KUWA KITOVU CHA UCHUMI BARANI AFRIKA


Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi barani Afrika.

Maalim aliyaeleza hayo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Alabama Michenzani Wilaya ya Mjini Unguja.

Maalim Seif alisema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa na bandari, ambayo wafanyabiashara wataweza kuingiza bidhaa zao bila ya ushuru na wakati wa kutoa watatozwa ushuru kidogo sana.

Alisema akilifanya hilo, wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki na Kati wataweza kuingia Zanzibar na kujipatia bidhaa zote wanazozitaka na ushuru utakuwa mdogo.

Maalim Seif kadhalika aliweka wazi kuwa katika miaka yake mitano atahakikisha Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ambalo ndege zake zitatembea duniani kote.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527