Katibu Mkuu Wa Mambo Ya Nje Afanya Mazungumzo Na Mratibu Mkazi Wa Umoja Wa Mataifa Nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Generali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,
Bw. Zlatan Milišić alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 2 Septemba 2020.

Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo Balozi Ibuge alitoa shukrani kwa Shirika hilo kwa ushirikiano uliopo kati yake na Serikali hususan kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Kwa upande wake, Bw. Milišić aliipongeza Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu ambao ni chanzo cha uchumi wa nchi kustawi.

 Pia aliipongeza kwa kuendelea kuchangia vikosi vya ulinzi wa amani kwenye mataifa mbalimbali  yenye  migogoro duniani na kuitakia Tanzania uchaguzi wa amani na utulivu hapo mwezi Oktoba 2020.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments