BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS KENYATTA

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. John Stephen Simbachawene.

Hafla ya kuwasilisha hati za utambulisho imefanyika Ikulu jijini Nairobi ambapo pamoja na mambo mengine, Rais Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Balozi Simbachawene. 

Balozi Simbachawene amemhakikishia Rais Kenyatta kuwa ataendelea kuboresha mahusiano ya nchi hizo mbili za Tanzania na Kenya, kukuza biashara baina ya nchi hizo kwa kuboresha diplomasia ya uchumi kwa ujumla wake.
 Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa tayari kupokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post