BWALO GYMNASTIC CENTRE YAENDESHA SHINDANO LA MBIO ZA MARATHON SHINYANGA


Washindi tano bora kwa wanaume na wanawake walioshiriki wameendesha mashindano ya mbio fupi za riadha kilomita 14 leo Shinyanga Mjini
***
Kikundi cha Wadau wa michezo mkoani Shinyanga ‘Bwalo Gymnastic Centre Shinyanga’ wameendesha mashindano ya mbio fupi za riadha 'Marathon ya Kwanza mkoani Shinyanga' kwa kukimbia umbali wa  kilomita 14 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya nusu Marathon ya mkoa wa Shinyanga.

Mashindano hayo ya mbio fupi za riadha yamefanyika leo Jumamosi Septemba 26,2020 zimeanzia katika uwanja wa Valleyball wa Risasi ulioko jirani na kituo kikuu cha polisi cha wilaya ya Shinyanga kupitia maeneo ya Ushirika hadi katika eneo la Kiwanda cha Fresho kilichopo Ibadakuli na kurudi uwanja wa Valleyball Risasi. 

Inaelezwa kuwa mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambayo haijawahi kushiriki,kushirikishwa wala kuandaa mbio za Marathon hivyo mbio hizo zilizofanyika leo zimetajwa kuwa ni mwanzo wa maandalizi ya mbio za kimkoa zinazotarajiwa kufanyika mwaka ujao malengo makuu yakiwa ni kuufanya mkoa uwe na wanariadha watakaoshiriki mbio za kitaifa na kimataifa. 

Miongoni mwa wadau wa michezo walioshiriki mbio hizo za Marathon ya Kwanza iliyoandaliwa na Bwalo Gymnastic Centre Shinyanga- BGC kwa kushirikiana na Mlezi wa BGC ACP Debora Magilimba ni askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga. 
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akiwa na washiriki wa mbio za Marathon leo Shinyanga


Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akiwa na washiriki wa mbio za Marathon leo Shinyanga
 

Washiriki wa mbio za Marathon wakipiga picha ya kumbukumbu.

Washiriki wa Mbio za Marathon wakikimbia
 

 
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akikabidhi zawadi kwa washiriki wa mbio za Marathon leo Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post