CHADEMA WAZINDUA RASMI KAMPENI JIMBO LA KISESA...GIMBI MASABA, KISHABI WANADI SERA


Makamu Mwenyekiti Chadema Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba akiwaombea kura wagombea wa CHADEMA

Na Mwandishi wetu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kimetikisa Jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu, Mkoa wa Simiyu, wakati wa uzinduzi kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Kisesa Francis Kishabi.

Akihutubia wananchi waliohudhuria mkutano huo leo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, Gimbi Masaba, amewaomba wananchi wa Kisesa kuwachagua wagombea wote wa CHADEMA ngazi ya Ubunge, urais na udiwani.

"CHADEMA tukishinda tutaondoa kero zinazowakabili wananchi wa Kisesa, ikiwamo ya kuvamiwa wanyamapori- tembo", amesema.

Mgombea Ubunge Jimbo la Kisesa, Francis Kishabi, akihutubia mkutanoni hapo ameahidi kushughulikia tatizo la maji, afya na kuboresha sekta ya kilimo na elimu zinazowatatiza wananchi wa eneo hilo.

Kulingana na mgombea Kishabi, ataweka mazingira rafiki ya elimu iwapo ataaminiwa kwenda kuwawakilisha bungeni. 

"Hakutakuwa na makosa katika uongozi wangu. Naomba nitumeni nikawatetee bungeni na kuwaletea maendeleo ya kisekta," Kishabi amesema.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kisesa ni Francis Kishabi akiomba kura kwa wananchi wa Kisesa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post