RAIS MAGUFULI KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KESHO


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Magufuli, Kesho Tarehe 06 Agosti, 2020 atachukua fomu ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya UchaguziTanzania (NEC) Njedengwa Jijini Dodoma.



Rais Magufuli atachukua fomu majira ya Saa tatu asubuhi na atasindikizwa na watu wachache wakiwemo viongozi wakuu wa Chama, ikiwa ni kutekeleza matakwa na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Rais Magufuli anachukua fomu hiyo ili kugombea Urais kwa kipindi cha Pili katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.

Baada ya kuchukua fomu, Rais Magufuli atakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma (White House) ambako atakutana na wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM na kuwasalimu. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527