KANGOYE ATAKA WENYEVITI WA MITAA, MABALOZI NA VIJANA KUENDELEZA MSHIKAMANO WAGOMBEA CCM WASHINDE KWA KISHINDO


Picha ya Jackson Kangoye akiongea na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM nyumbani kwake


Na Mwandishi wetu - Tarime

Wenyeviti wa mitaa, mabalozi vijana pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi jimbo la Tarime mjini wameaswa kuendeleza ushirikiano na kuvunja makundi ili mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki aweze kushinda kwa lengo la  kuleta maendeleo.

 Kauli hiyo imetolewa na Jackson Kangoye ambaye alishinda kwenye kura za maoni Jimbo la Tarime mjini katika hafla fupi aliyoandaa kwa ajili ya kutoa shukrani zake kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi.

Jackson alisema kuwa ameamua kuandaa hafla hiyo ya pamoja kwa ajili ya kushukuru wajumbe wa Halmashauri kuu kwa kumchagua kwa kura nyingi licha ya jina lake kutorudi lakini bado ataendelea kupigania Chama Cha Mapinduzi mpaka kinashika dola katika majimbo yote mawili ya Tarime mjini na vijijini.

“Najua hapa kuna wenyeviti wa mitaa hawapigi kura katika mkutano wa Halmashauri kuu lakini walishawishi wajumbe kwamba tunaomba mkapigie flani kuna vijana, wanachama wote nimeamua kuwaita kujumuika na nyie kuwambia mimi niko pamoja na mgombea aliyeteuliwa na chama naheshimu maamuzi ya cha kuanzia ngazi za kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa”,alisema Jackson.

Pia Jackson aliongeza kuwa hayupo tayari kuhamia chama chochote kwa sababu amelelewa ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwani amekuwa akipokea simu mbalimbali kutoka vyama tofauti wakimshawishi kugombea kupitia vyama hivyo.

“Nimepigiwa simu sana kwenda vyama vingine lakini nimeheshimu wanachama wa jimbo la Tarime mjini kwa kuwa walinihamini hivyo siwezi kuangusha wazee wangu nimelelewa na chama hiki sitaweza kuwa msaliti”,alisema Jackson.

Aidha Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwemo wazee maarufu wamedai kuwa Ushirikiano Umoja na Upendo utachangia kwa kiasi kikubwa Ushindi.

Pia Wanachama hao wamempongeza Jackson kwa kitendo cha kuwaita wanachama wote ili kushiriki chakula cha pamoja jambo ambalo limewashangaza na kuzidi kusema kuwa kijana huyo ni mkomavu wa siasa kwani baadhi ya wagombea wamekuwa wakishindwa kurejea baada ya kutoteuliwa na chama.

Chama cha Mapinduzi Jimbo la Tarime Mjini wanatarajia kufungua rasmi kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki hii leo  Agosti 30 katika viwanja vya soko la zamani mjini Tarime ambapo Kangoye amehaidi kushiriki kikamilifu kumtafutia kura mgombea huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post