IDADI YA WATOTO WANAONYONYESHWA MAZIWA YA MAMA PEKEE BAADA YA KUZALIWA NCHINI NI ASILIMIA 58


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 28 ya wiki ya unyonyeshaji duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt Germana Leyna akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua kitini cha lishe ya wanawake,watoto na vijana balehe wakati wa maadhimisho hayo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi Mwakilishi wa Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga Burhan Yakub kitini cha lishe ya wanawake,watoto na vijana balehe wakati wa maadhimisho hayo kwa ajili ya waandishi wa habari



WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akisoma vipeperushi mbalimbali kwenye banda la worldvision wakati wa maadhimisho hayo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na watu mbalimbali wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jitegemee

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye Picha ya pamoja wakati wa maadhimisho

Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo




TAKWIMU za hali ya ulishaji watoto nchini zinaonyesha idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee nchini bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vyengine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 58.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 28 ya unyonyeshaji duniani iliyofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza.

Ambapo alisema pia watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi katika kipindi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 53.

Waziri Ummy alisema idadi yao wanaoanzishiwa vyakula vya nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi sita hadi nane ni asilimia 87

“Lakini pia idadi watoto wenye umri wa miezi 6-23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni asilimia 36 vigezo hivyo ni idadi sahihi ya milo anayopewa mtoto kwa siku kulingana na umri wake na uwe na mchanganyiko wa vyakula kutoka kwenye makundi yasiyopungua manne ya vyakula”Alisema

Alisema ili kuboresha viwango vya unyonyeshaji na ulishaji watoto vyakula vya nyongeza ,kila mmoja ana wajibu wa kufanya jambo Fulani katika azimio la Inocenti la mwaka 1990 nchi zilikubaliana mambo mbalimbali ya kuyasimamia makubaliano.

Alieleza kwamba makubaliano hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa zahanati, vituo vya aafya na hospitali zinazotoa huduma za ukunga zinatoa huduma bora za kufanikisha unyonyeshaji maziwa ya mama.

Alizitaja baadhi ya hizo ni pamoja na kutoa elimu ya unyonyeshaji na lishe ya watoto kwa jamii lakini pia kuhakikisha wanawake wanaojifungua waanze kuwanyonyesha watoto wao mapema ndani ya saa moja baada ya kujifungua.

“Lakini pia kuwafundisha wanawake waliojifungua jinsi ya kumpakata na kumweka vizuri mtoto kwenye titi baada ya kujifungua na jinsi ya kukamua maziwa ya mama”Alisema Waziri Ummy.

Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt Germana Leyna alisema kila mwaka dunia nzima inasheherekea wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

Alisema shehe hizo zilianza rasmi 1991 na nchi iliridhia na kuona ni jambo nzuri lengo kubwa la wiki hii ni kuhamasisha wakina mama kuwanyonyesha watoto chini ya miezi sita maziwa ya mama pekee.

Dkt Germana alisema wanahamasisha jambo hilo kwa sababu maziwa ya mama yanampa mtoto virutubisho vyote vya lishe anavyohitija kwenye miezi sita ya awali.

Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani kwa mwaka 2020 yamebabwa na kauli mbiu inayosema “Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527