PATROBAS KATAMBI KESHO KUCHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI,KISHA KUSALIMIANA NA WANANCHI, CCM | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 21, 2020

PATROBAS KATAMBI KESHO KUCHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI,KISHA KUSALIMIANA NA WANANCHI, CCM

  Malunde       Friday, August 21, 2020

Patrobas Katambi

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mgombea wa Nafasi Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi (CCM) amewasili mkoani Shinyanga ambapo kesho Jumamosi Agosti 22,2020 atachukua Fomu ya Kugombea Ubunge kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini tayari kwa kuanza rasmi mchakato wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020. 

Akizungumza na Malunde 1 blog, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Said Bwanga amesema Katambi ambaye ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM taifa (NEC) kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, atachukua Fomu kesho majira ya saa tatu asubuhi katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini. 

“Mgombea Ubunge Patrobas Katambi tayari amewasili Jimboni na kesho anatarajia kuchukua fomu kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini akisindikizwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Madiwani walioteuliwa kupeperusha Bendera ya CCM katika uchaguzi Mkuu 2020 na Watia nia kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini mwaka 2020”,amesema Bwanga. 

Amesema mara baada ya kuchukua fomu, Katambi ataelekea katika Ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa ajili ya kusalimiana na wanachama wa CCM na wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post