ZITTO KABWE AMKARIBISHA BENARD MEMBE ACT - WAZALENDO | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 1, 2020

ZITTO KABWE AMKARIBISHA BENARD MEMBE ACT - WAZALENDO

  Malunde       Wednesday, July 1, 2020

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amemkaribisha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mwanachama wa CCM Bernard Membe, kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala hii ni mara baada ya yeye kufukuzwa uanachama ndani ya CCM.Akizungumza jana  na mamia ya wafuasi wa chama hicho, katika eneo la Njia Nne, wilayani Kilwa, mkoani Lindi, Zitto alisema, anamkaribisha Membe ndani ya ACT- Wazalendo kwa mikono miwili

“Tunamtaka Membe kujiunga na chama chetu, ili kuihami demokrasia na kupigania haki za wananchi,” alieleza Zitto na kuongeza, “mtu yoyote anayeona ukandamizaji haufai, anapaswa kuungana na wenzake, kupinga vitendo hivyo.

"Ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko ni hatua sahihi, hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala"


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post