WAKENYA WAMLILIA RAIS MSTAAFU WA TANZANIA BENJAMIN MKAPA


CHAMA cha upinzani nchini Kenya cha Orange Democratic Movement(ODM) kupitia kiongozi wake Raila Odinga kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa.

Rais mstaafu Mkapa amefariki dunia leo Julai 24 na taarifa za kifo chake zimetangazwa na Rais Dk.John Magufuli na kwamba taarifa nyingine zitaendelea kutolewa hapo baadae.

Kutokana na taarifa hizo za kusikitisha Odinga kwa niaba ya Chama chake amesema Mkapa alikuwa rafiki mkubwa wa watu wa Kenya na muumini mkubwa wa Pan Africanism pamoja naha  ushirikiano wa Kusini-Kusini.

Amesema hakika Taifa la Kenya linabaki na kumbukumbu kubwa ya Mkapa kwa jinsi ambavyo alisimama kidete katika kuhakikisha amani ya nchi yao inarejea baada ya kuibuka kwa vurugu zilizotokana na uchaguzi Mkuu mwaka 2007 hadi mwaka 2008.

"Wakenya tutaendelea kubakiwa na kumbukumbu kubwa kwa namna ambavyo Mkapa alivyohusika kwa kushirikiana na Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan pamoja na Graca Machel katika kusaidia kurudisha amani nchini kwetu iliyotoweka kutokana na ghasia za uchaguzi mkuu,amesema Odinga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527