MAGUFULI APITISHWA KWA KISHINDO KUWA MGOMBEA URAIS 2020 KUPITIA CCM


John Magufuli kwenye Mkutano Mkuu

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, wamempitisha Ndugu John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kwa kura 1822.

Mkutano huo umefanyika leo Julai 11, 2020 kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma na kuhudhiriwa na wajumbe wa kamati kuu pamoja na wageni mbalimbali waalikwa kutoka nje na ndani ya nchi.

Akitangaza matokeo ya kura hizo mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi ambaye ni Spika wa Bunge Mh Job Ndugai amesema idadi ya wajumbe waliohudhuri ni 1822 na hakuna kura iliyoharibika hivyo ameshinda kwa asilimia 100.

Sasa rasmi CCM imekamilisha mchakato wa kupata wagombea kwa ngazi ya Urais ambapo kwa Zanzibar atasimama Hussein Mwinyi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atasimama Rais Magufuli anayeingia katika awamu yake ya pili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527