BINTI WA NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA


Zindzi Mandela, binti ya marehemu shujaa, Nelson Mandela amefariki dunia. 

Zindzi ambaye amefariki mjini Johannesburg mapema leo Jumatatu, Julai 13 akiwa na miaka 59, alihusika katika vita vya kupigania uhuru nchini Afrika Kusini. 

Kabla ya kifo chake, Zindzi alihudumu kama balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark. 

Marehemu Zindzi alizaliwa mnamo Disemba 23, 1960 huku siku yake ya kuzaliwa ikiwa wakati ambapo baba yake alikamatwa na kuhukumiwa miaka 27 gerezani. 

Mandela alitumikia kifungo chake kisiwani Robben Island, katika Gereza la Pollsmoor naVictor Verster baada ya kuhukimiwa kwa kujaribu kupindua serikali. 

Wakati akitimza umri wa miaka 17, mama yake alipigwa marufuku nchini humo kwa miaka 8 na hii ndio mojawapo ya sababu zake kupigania uhuru. 

Alikuwa maarufu mwaka 1985 wakati alisoma taarifa ya baba yake akiwa gerezani katika uwanja wa Jabulani, Soweto ambapo alimsuta aliyekuwa rais wakati huo Pieter Willem Botha kwa uongozi duni. Marehemu amewaacha watoto wanne na mume.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527