WATATU WATIWA MBARONI DAR ES SALAAM KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA DEREVA TAX (UBER) | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 4, 2020

WATATU WATIWA MBARONI DAR ES SALAAM KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA DEREVA TAX (UBER)

  Malunde       Thursday, June 4, 2020
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya dereva tax (UBER) aliyefahamika kwa jina la Joseph Tillya Mpokala,(51),Mkazi wa Mbezi kwa Msuguli.

Watuhumiwa hao :-

1. Godson Laurent Mzaura,(29),Mkazi wa Mbezi Beach,Mpiga picha.

2. Said Mohamed Mahadhi (38),Mkazi wa Afrikana,Fundi simu na

3. Denis Urassa @ Pasua,(45),Mkazi wa Makongo Juu,Fundi simu.

Mnamo tarehe 26.05.2020 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm lilipata taarifa kutoka kwa mke wa marehemu kuwa Mume wake ametoweka tangu tarehe 21.05.2020 na simu zake zote hazipatikani.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM kupitia kikosi chake cha kupambana na uhalifu kilianza ufuatiliaji mara mmoja.

Mnamo tarehe 27.05.2020 alikamatwa mtuhumiwa Godson Laurent Mzaura na kuhojiwa kisha kukiri kufanya mawasiliano na marehemu ambapo alieleza kuwa Mnamo tarehe 21.05.2020 majira ya saa saba mchana walimkodi marehemu ili awapeleke maeneo ya Mbezi na walipofika Mbezi Juu watuhumiwa hao walimuua Joseph Tillya na kumfukia kwenye shimo katika eneo la wazi lenye uzio wa ukuta ambao hujamalizika kujengwa(pagale).

Mnamo tarehe 02.06.2020 watuhumiwa Wote watatu walihojiwa kwa kina na kukiri kuwa walifanya mauaji hayo na kuchukua gari la marehemu lenye T 139 DST Toyota IST na kwenda kulificha huko Kimara Baruti katika nyumba ya wageni ya Api Forest logde.

Jeshi la Polisi kanda Maalum DSM linakamilisha taratibu za kupeleka jalada kwa mwasheria wa serikali na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Imetolewa na Kamanda wa Polisi,
Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
SACP-Lazaro Mambosasa,
03/06/2020


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post