SHULE ZOTE NA VYUO VIKUU NCHINI KENYA KUENDELEA KUFUNGWA HADI MWEZI WA TISA KWA MADAI YA KUKABILIANA NA CORONA

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuendelea kufungwa kwa  shule na vyuo vikuu nchini Kenya hadi Septemba Mosi mwaka huu ambapo vitafunguliwa tena.


Akilihutubia taifa kutoka ikulu ya rais jijini Nairobi rais Kenyatta anasema kuwa amechukua hatua hiyo ili kulinda maisha ya wanafunzi na  walimu haswa kutokana na idadi kubwa ya maambukizi aya COVID 19 yanayoendelea kupanda.

Rais Uhuru kenyatta aidha ametangaza kuongezwa kwa muda wa marufuku ya kutoka nje kwa mwezi mmoja zaidi amri iliyotangazwa na serikali kudhibiti maambukizi ya Corona ila muda wa utekelezwaji wake ukibadilishwa na kuanza saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527