SERIKALI YATISHIA KUKIFUTA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI


Serikali imetishia kukifuta chama cha wafugaji nchini kutokana na kukaidi maelekezo yaliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani kuhusu maandalizi ya kuelekea uchaguzi wa viongozi wa chama hicho unaotaraji kufanyika Julai mwaka huu ambapo baadhi ya viongozi wa chama hicho wanadaiwa kuhusishwa na njama za kukwamisha uchaguzi huo.

Tamko la serikali limetolewa na naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani Bw. Ramadhan Kailima alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofsi ya chama hicho iliyopo jijini Dodoma na kukuta ikiwa imefungwa hali inayokwamisha maandalizi ya uchaguzi huo ambapo wanachama wanapaswa kufika katika ofisi hizo kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi.

Awali uchaguzi huu ulipangwa kufanyika tangu mwishoni mwa mwaka 2018 lakini ulikwama kutokana na kutokuwepo na maelewano baina ya wanachama.

Kwa upande wake afisa sheria ofisi ya msajili wa jumuiya kutoka wizara ya mambo ya ndani Bw. Eliud Mwailafu amesema mpaka sasa hakuna maandalizi yoyote yaliyofanywa ya kuelekea uchaguzi wa viongozi wa chama licha ya waliokuwepo kumaliza muda wao tangu mwaka 2018.

Tayari wizara ya mambo ya ndani ya nchi ilikwisha toa maelekezo kwa viongozi waliopo katika chama hicho kuwa uchaguzi ufanyike Julai 16 mwaka huu 2020.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527