SERIKALI YA MAREKANI YATOA DOLA MILIONI 3.6 KUPAMBANA NA COVID-19 TANZANIA


 
Serikaliya Marekani imetenga kiasi cha dola millioni3.6 ( Shilling billioni  7.8) kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Tanzania katika mapambano dhidi ya janga la Korona (COVID-19).

Pia serikali hiyo imetoa kiasi cha dola millioni 1.9 ( shilingi Billioni 4.4) kupitia shirika lake la msaada la USAID ili kuisaidia Tanzania kukabiliana na mlipuko huo.

Mwakilishi Mkazi wa shirika la USAID
nchini Tanzania Andy Karas alisema haya katika mkutano wake na waandishi wa habari. Alisema kuwa kuwa ni jambo la muhimu sana kuendeleza juhudi nyingine za kusaidia huduma za afya hata kipindi cha mlipungu wa janga hili la COVID-19

“ Kiasi hiki kinakadiriwa kuwa jumla ya dola
milioni 5.3 ambazo zilitolewa katika programu ya rasilimali,
Mawasiliano kuhusu athari ya magonjwa kuboresha mawasiliano, upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira Kudhibiti na kuzuia maambukizi zaidi,”

“Ukijumuisha msaada wa pesa mpya na pesa kutoka miradi mingine zilizobadilishiwa kazi, jumla inakuwa ni dola za kimarekani milioni 5.3 (sawa na shilingi
bilioni 12.2 fedha za kitanzania).,” Alisema Karas .

Alielezea zaidi kuendelea kujitoa ili kushirikiana na kusaidiana na jamii ili kuhakikisha kuwa rasilimali za kutosha zinawekezwa kusaidia mapambano dhidi ya COVID 19 nchini.

Karas alisema kuwa msaada huo kwa Tanzania, ni sehemu ya takribani dola billioni 6.5 zilizotolewa na watu
wa serikali Marekani na wasio wa serikali ikiwa ni msaada wa jumla kwa dunia ili kusaidia mwitikio wa COVID-19 ambapo msaada huo ni sawa na asilimia 60 ya jitihada kwa dunia nzima.

Mkurugezi mkazi wa USAID pia alielezea ahadi na utayari wa Serikali ya Marekani ya kuendelea kuishauri Serikali ya Tanzania ili kuweza kushinda vita dhidi ya COVID-19 Kituo cha Kudhibiti na kuzuiaMagonjwa (CDC)

Kwa upande mwingine, Karas alidhihirisha msaada mkubwa uliotolewa na Kituo cha Kupambana na Magonjwa (The U.S. Centers for Disease Control and Prevention (CDC)ambacho kimetoa dolla milioni 3 katika mfuko mpya fedha
zake na kutenga zaidi ya dola 600,000 katika fedha zake zilizokuwa
zimepangwa kwa matumizi mengine ili kuunga mkono katika uchunguzi, maabara, na kuzuia na kupambana na maambukizi ya CIVID 19 nchini Tanzania.

Alisema kuwa CDC itaendelea kutafuta njia bunifu ili
kusaidia juhudi za mwitikio hasa msaada wa kiufundi na usimamizi huduma za afya za Mikoa na Wilaya. Na kuwa kwa sasa CDC inasaidia  maeneo yafuatayo:

Aliongeza kuwa CDC inaendelea kutafuta njia za
ubunifu kusaidia juhudi za kukabiliana na janga ikiwa ni pamoja na
kusaidia walengwa ambao ni timu ya wataalamu wa afya ngazi ya
mkoa/wilaya. Jitihada zilizofanywa na CDC ni pamoja na:

CDC ilikuwa imejikita katika uchunguzi wa wagonjwa wa kwanza wa COVID-19 nchini Tanzania (bara na Zanzibar). Ilitoa msaada wa rasilimali za uchunguzi, mikakati na interventions.

Pia, Timu ziliandaliwa katika mikoa mbali mbali ili kuleta mwitikio na kutoa msaada wa kitaalamu. Pamoja na kazi nyingine, timu ziliendelea kufanya uchunguzi, contact tracing tools

Kwa upande wa ufanisi wa upimaji wa
COVID-19, zaidi ya dolla milioni 1.8 imetengwa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maabara nchini, ambapo takribani dolla 270,000 imekwisha tolewa kwa ajili ya vifaa vya maabara, na uchunguzi.

Athari za COVID-19 (Kwa sekta mbalimbali)
Kutokana na madhara ya maradhi ya COVID-19 na usitishwaji wa ndege za kimataifa, uuzaji wa mazao ya matunda na mboga mboga ( horticultural products) ulisitishwa kwa muda, na kusababisha madhara katika uzalishaji na ajira.

Bidhaa nyingi za matunda na mboga mboga
nchini Tanzania, huandaliwa kwa ajili ya usafirishaji nje ya nchi
(export market), ambapo uhitaji (demand) ni mkubwa kuliko uzalishaji (suppy), hivyo  USAID inawekeza katika taasisi ya Tanzania Horticultural Association (TAHA) na Serikali ya Tanzania.

Juhudi pia zinahusisha kutoa muda wa maongezi kwa walimu upima na kusambaza  ujumbe juu ya uzuiaji wa COVID-19 (ikihusisha usafi),Ukatili kinyume na wanawake na wasichana unaongezeka kidunia huku kukiwa na maradhi COVID- 19, Tanzania haina tofauti na nchi nyingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527