HII HAPA RATIBA YA MCHAKATO WA KUWAPATA WAGOMBEA WA CCM WA NAFASI YA RAIS WA TANZANIA NA RAIS WA ZANZIBAR KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020

 3.0.     MAMBO YA KUZINGATIWA NA KILA MGOMBEA
(i)         Kila mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lazima apate wadhamini 250 katika Mikoa 12 angalau Mikoa 2 kati ya hiyo iwe ya Zanzibar.


(ii)        Kila mgombea wa Urais wa Zanzibar ni lazima apate wadhamini 250 katika Mikoa isiyopungua mitatu, kati ya hiyo angalau Mkoa mmoja kutoka Unguja na mmoja kutoka Pemba.

(iii)      Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(iv)      Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais wa Zanzibar.

(v)       Mwanachama haruhusiwi kumdhamini mgombea zaidi ya mmoja.

(vi)      Fomu ya udhamini ya wanachama ithibitishwe na Katibu wa CCM wa Wilaya kwa kupigwa muhuri wa chama wa Wilaya husika.

(vii)    Wanachama watakaomdhamini mgombea, uanachama wao uthibitishwe na Katibu wa CCM wa Wilaya husika.

(viii)   Kila mgombea atalazimika kuzingatia maadili ya Chama Cha Mapinduzi, masharti ya uongozi, sifa za wagombea na utaratibu wa kuomba uongozi kama ilivyofafanuliwa katika Kanuni za Uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya Dola, Kanuni za Uchaguzi na Kanuni za Uongozi na Maadili.

4.0    TAARIFA YA ZIADA
(i)      Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi ya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Kata/Wadi na Viti Maalum kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 watachukua na kurejesha fomu kati ya tarehe 14 na 17 mwezi Julai 2020. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 17/07/2020 Saa 10.00 jioni.

(ii)     Taarifa rasmi ya mchakato wa kuwapata wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Kata/Wadi na Viti Maalum kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 itatolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi tarehe 11/07/2020.
      
MFULULIZO WA MATUKIO YA RATIBA YA MCHAKATO WA KUWAPATA WAGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WA NAFASI YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA RAIS WA ZANZIBAR KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post