WAKULIMA WA MPUNGA KAHAMA WASHAURIWA KUUNDA AMCOS

 Kaimu Mrajis wa mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace katikati akiwa juu ya mpunga ulio katika ghara la nje nyumbani kwa mkurugenzi wa Nyanhembe Agricultural Farm Bw. Khamis Mgeja, wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kahama KACU, Emmanuel Charahani, na kulia ni  mkulima wa mpunga  Bw.Khamis Mgeja ambaye ni mkurugenzi wa Nyanhembe Agriculture Farm.

 *****
Wakulima wa zao la mpunga Wilayani Kahama,mkoani Shinyanga wameshauriwa kujiunga pamoja na kuanzisha AMCOS zinazonunua mazao ya mpunga kitakachopelekea kuanzishwa kuundwa kwa Chama Cha Ushirika wa Zao la Mpunga ili kuwawezesha kuuza mazao yao kwa bei yenye tija kwani umoja ni nguvu.

Akizungumza juzi na wakulima wa zao hilo Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Shinyanga, Hilda Boniphace mara baada ya kuwatembelea wakulima wa zao la mpunga katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya kilago wilayani Kahama, aliwataka kuanzisha AMCOS itakayoshilikiana na Chama Kikuu cha Ushirika KACU ili ijishughulishe na ununuzi wa zao la mpunga.

“Niseme tu hawa walanguzi wameanza kupita siku nyingi kwa wakulima mashambani na kwamba mbali na zao la mpunga pia tumesikia walanguzi hao wanalangua mazao mbalimbali hivyo serikali haitawavumili, niwaombe tu wakulima msikubali kulanguliwa kiholela na uzuri wa mpunga unatunzika na ndiyo maana uwekewe utaratibu wa mfumo wa stakabadhi gharani,” alisema Mrajis msaidizi.

Aidha Hilda alibainisha kuwa kumekuwa na taarifa za wakulima kunyanyaswa na walanguzi wa zao hilo ambapo wanadaiwa kwenda moja kwa moja mashambani wakiwa na ndoo kubwa za jina maarufu muzambiki lililopanuliwa kwa kuchemshwa kwa mafuta na maji ya moto ili litanuke zaidi badala ya kutumia kipimo cha mizani halali lengo ni kuwapunja wakulima wa mpunga na kupelekea kutonufaika na kilimo chao.

Kabla ya kufanya ziara fupi mashambani ili kuonana na wakulima wa mpunga, Kaimu Mlajis alitoa maagizo na ushauri alipokutana na jopo la wazee la Wilayani Kahama (UWAKA) likiongozwa na Mwenyekiti Nathan Omgani na katibu wa umoja huo Paul Ntelya na baadhi ya wakulima wakiongozwa na Khamis Mgeja katika kikao cha mashauriano kilichofanyika katika kiwanda cha kuchambulia pamba cha Kacu Ukumbi wa Charahani Hall eneo la Mhongolo wilayani Kahama.

Katika kikao hicho cha ndani cha mashauriano kilikuwa pia na wajumbe wa bodi ya chama cha ushirika wilayani Kahama Kacu menejmenti, maafisa Ushirika wa Halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo Mrajisi huyo aliwaeleza wazee na wakulima hao kuwa serikali kwa upande wake ipo pamoja na wakulima inahakikisha wakulima siku zote wananufaika na kilimo chao ndiyo maana inaelekeza mpango wa stakabadhi gharani.

Baada ya kikao cha mashauriano, mrajis huyo pamoja na bodi ya Kacu alishauri wote waongozane kwenda kijijini kuona maendeleo ya mashamba ya mpunga ikiwa ni pamoja na kusikiliza changamoto zainazowakabili wakulima huko huko mashambani.

Akizungumza wakati wakiwa mashambani katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya kilago wilayani Kahama naye Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kacu Emmanuel Charahani aliyeongozana na bodi nzima, alisema kuwa chama chake kimejipanga kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya mpunga na kuandaa kibali kutoka kwa Mrajis na bajeti ya kununua hilo.

Hata hivyo baadhi ya wakulima wa zao hilo akiongea kwa niaba ya wakulima hao Khamis Mgeja ambaye ni mkurugenzi wa Nyanhembe Agriculture Farm akizungumzia suala la mateso wanayokabiliana nayo ni pamoja na wakulima kutonufaika na zao hilo kutokana na wimbi la walanguzi uchwala wanaokuja na ndoo za mozambiki jambo ambalo ni kuwapunja wakulima na ni unyonyaji mkubwa.

Mgeja pia kwa niaba ya wakulima walimpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kusikiliza kilio cha wanyonge wakulima wa zao la mpunga mkoani Shinyanga na kutoa maagizo ya ushauri wasiwakubalie walanguzi kuwanunulia m,ashambani badala yake aliwataka watunze mazao yao ili baadaye wauze kwa bei nzuri.

“Ushauri huo wa Mheshimiwa Rais sisi wakulima wa zao la mpunga tumeupokea kwa mikono miwili na kuanza kuuzingatia kwani Mheshimiwa Rais siku zote anania njema na wakulima wote wa Tanzania kwani yeye siku zote ni mtetezi wa wanyonge,”alisema Khamis Mgeja.

Kutokana na hali hiyo pia Mgeja aliwapongeza bodi ya Kacu na menejiment yake pamoja na Kaimu Mrajis Hilda Boniphace kuondokana na umangimeza wa kukaa maofisini tu kwa kuwatembelea wakulima mashambani na kuona maendeleo na changamoto za wakulima na kuahidi kuendelea kuzingatia maagizo, Ushauri na maelekezo yanayotolewa na serikali kwa wakulima.
 Kaimu Mrajis Hilda Boniphace akizungumza na baadhi ya wakulima alipotembelea kwenye mashamba yao ya mpunga katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya kilago wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
kushoto kaimu Mlajis Hilda Boniphace na mwenyekiti wa KACU Emmanuel Charahani wakipepeta mpunga baada ya kufika nyumbani kwa mkulima Khamis Mgeja katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya Kilago Wilayani Kahama Mkoani shinyanga.
Baadhi ya wakulima wa mpunga katika kijiji cha Nyanhembe kata ya Kilago wialayani Kahama mkoani shinyanga wakiwa katika mashamba yao ya Mpunga huku wakifurahia kutembelewa na kaimu Mlajis Bi. Hilda Boniphace pamoja na uongozi mzima wa bodi ya KACU ukiongozwa na Mwenyekiti wake Emmanuel Charahani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527