MAKADA 15 CCM WAREJESHA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, June 27, 2020

MAKADA 15 CCM WAREJESHA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

  Malunde       Saturday, June 27, 2020
Wanachama 15 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamerudisha fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kuzijaza na kudhaminiwa.

Hadi jana Ijumaa tarehe 26 Juni 2020, takribani makada 15 kati ya 30 waliojitokeza kugombea nafasi hiyo, walirejesha fomu za kugombea urais wa Zanzibar.

Waliorudisha fomu ni, Balozi Ali Abeid Karume, mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume. Dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Ulinzi na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Ali Hassan Mwinyi.

Wengine ni, Shamsi Vuai Nahodha, aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Zanziba. Mhandisi Makame Mbarawa, Waziri wa Maji. Mbwana Bakari Juma, Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Shehe Mussa, Mohamed Hijja Mohamed , Mohamed Jumanne ,Issa Suleiman Nassor, Abdulhalim Mohamed Ali, Khamis Mussa Omar, Rashid Ali Juma, Dk. Khalid Salum Mohamed, na Ayoub Mahmoud Mohamed.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post