AUA WAKWE ZAKE 'MME NA MKE' KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA 'WANAMROGA'

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kijana aliyejulikana kwa jina la Patrick Ngailo mkazi wa Mlangali wilayani Ludewa mkoani Njombe,anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya wakwe zake (mme na mke) akiwatuhumu ni washirikina wanaomsababishia maradhi ya mara kwa mara.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema kijana huyo alitenda kosa hilo katika kijijji hicho June 8,2020 majira ya saa moja jioni lakini wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamemkamata kijana huyo.

“Baada ya kufanya maauaji haya huyu mtu alikimbia lakini wananchi walishilikiana na jeshi la polisi alikamtwa na sheria inafuata mkono wake”

Awali kamanda Issa alisema jeshi hilo limefanya uchunguzi na kubaini kuwa Ngailo alioa mtoto wa wazee hao lakini akapatwa na maradhi ya mara kwa mara na kuchukuwa uamuzi wa kwenda kwa mganga alikoelezwa kuwa anapata maradhi kutokana na mke wake.

“Awali alioa mtoto wao baada ya kuoa mtoto huyo alienda kwa mganga kutokana na kuumwa umwa na akajulishwa yeye anaumwa kwasbabu ya huyo mwanamke aliyemuoa akaamua kumuacha yule mwanamke,lakini cha ajabu kilichotokea alikuwa anaendelea kuumwa na alichokifanya aliamua kwenda kufanya mauaji ya mke na mume”alisema kamanda Issa

Aidha katika tukio jingine kamanda Hamis amesema lipo tukio jingine lililotokea hivi karibuni mkoani Njombe la kuuawa kwa mwanaume mmoja kutokana na kushambuliwa na vitu vyenye ncha kali akiwa amelala hali iliyofanya jeshi hilo kuwashikilia mama na watoto wa familia hiyo.

“Kuna tukio jingine la mauaji yenye utata ambalo baba na mama walilala katika nyumba moja lakini vyumba tofauti na asubuhi walipoamka baba alikuwa amefariki na kufariki kwenyewe kumetokana na kushambuliwa na vitu vyenye ncha kali,na hivi tunavyoongea mama na watoto wameshikiliwa kwa kuwa mauaji hayo yanaonekana yamefanywa na wanafamilia,jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na ukikamilika wahusika tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria”alisema kamanda


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post