WAISLAMU WATINGA KANISANI KUSALI MWEZI WA RADHAMANI....HISIA ZA AJABU ZATAWALA WAISLAMU NA WAKRISTO | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, May 24, 2020

WAISLAMU WATINGA KANISANI KUSALI MWEZI WA RADHAMANI....HISIA ZA AJABU ZATAWALA WAISLAMU NA WAKRISTO

  Malunde       Sunday, May 24, 2020

Kanisa moja kubwa mjini Berlin nchini Ujerumani limefungua milango kwa ajili ya Waislamu kusali kwa sababu hawawezi kutosha msikitini wakifuata utaratibu mpya wa kutokaribiana.

Ujerumani iliruhusu sehemu za kuabudiwa kufunguliwa Mei 4, lakini kwa masharti kuwa watu wakae kwa umbali wa mita 1.5 (5ft).

Na hii kupelekea msikiti wa Dar Assalam uliopo mjini Neuk├Âlln kushindwa kumudu vigezo hivyo kwa sababu hauwezi kutosha.

Lakini kanisa la Kilutheri la Martha katika mji wa Kreuzberg limetoa ruhusa kwa Waislamu kufanya ibada zao Ijumaa na katika wiki ya mwisho ya mfungo wa Ramadhani.

Kwa kipindi cha mwezi mzima wa Ramadhan, Waislamu wamekuwa wakijinyima kula, kunywa, kuvuta sigara na ngono kuanzia alfajiri hadi jioni.

Kwa kawaida familia na marafiki huwa wanajumuika kwa pamoja kuhitimisha mfungo kwa kusheherekea na kujumuika katika sala za pamoja, lakini kwa mjini Berlin - na hata maeneo mengi duniani sherehe hizo bado zimeathirika.
"Ni ishara njema na inaleta furaha kwa wakati huu wa Ramadhan na inaleta furaha katikati ya janga," Imamu mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters. "Mlipuko huu umetufanya kuwa jumuiya moja. Majanga yamewafanya watu wawe kitu kimoja."

"Ni hisia ya ajabu kwa sababu ya ala za muziki na picha za ukutani ni kitu tofauti," alisema muumini mmoja, Samer Hamdoun, hakuna kitu ambacho kinawakilisha swala za kiislamu."

"Lakini unapoangalia, unaposahau kidogo. Hii ni nyumba ya Mungu."
Hata wachungaji wa kanisa wamehudhuria swala hizo.

"Nilitoa hotuba Ujerumani," alisema Monika Matthias. "wakati wa maombi, nilikuwa naweza kusema ndio, ndio, ndio kwasababu tunamatatzio ya kufanana na tunataka kujifunza kutoka kwenu. Na hisia hiyo ni nzuri kati yetu."

Soma Zaidi <<HAPA>>
 CHANZO - BBC SWAHILI
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post