WATANZANIA WALIOKWAMA AFRIKA KUSINI KWA LOCKDOWN WAREJEA NYUMBANI


Na Mwandishi Maalumu
Balozi wa Tanzania nchini Afrka Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi Jumatatu Mei 25, 2020 amesimamia zoezi la repatriation (usafirishaji) wa dharura) ya Watanzania pamoja na raia kadhaa wa nchi hiyo waliokwama kutokana na Lockdown na kusitishwa safari za ndege inayoendelea huko, kutoka Johannesburg kuja Dar es salaam.


Taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini humo zinasema kwamba Balozi Milanzi aliratibu na kusimamia zoezi hilo ambapo Watanzania 14 ambao walikwama nchini humo kwa miezi miwili kufuatia Lockdown hiyo.

Raia 12 wa Afrika Kusini pamoja nna raia mmjoa wa Uingereza nao wakajiunga kwenya msafara huo baada ya kuona ni afadhali warejee Tanzania ambako hakuna Lockdown ili kuendelea kufanya kazi kwenye makampuni na taasisi za nchi hiyo.


Akiwasindikiza abiria hao walioondoka kwa ndege ya kukodi ya kampuni ya AS SALAAM AIR ya Zanzibar, Balozi Milanzi aliwapa pole kwa kuwa katika Lockdown ya miezi miwili na kuwatakia safari njema na maisha ya furaha watakapowasili Tanzania ambayo ni nchi pekee ambayo imekuwa namsimamo thabiti wa kupambana na gonjwa la COVID 19 lililosababisha nchi zingine kufungia kila mtu ndani.

Hili ni tukio la tatu la repatriation tokea gonjwa hilo liikumbe dunia
 na kusababisha sintofahamu kila pembe, kufuatia zile safari za India na Falme za Kiarabu ambapo serikali ilituma ndege maalumu kwenda kuchukua wananchi wake waliokwama huko kutokana na Lockdown katika nchi hizo.

Zoezi hilo limekuja wakati Tanzania imefungua rasmi anga lake na
kuruhusu utalii pamoja na safari za ndege za kimataifa viendelee kama kawaida, ambapo tayari mamia ya watalii wameendelea kumimimika nchini, huku wengine wakitarajiwa kuwasili kwa wingi baada ya mashirika ya ndege ya kimataifa kuanzisha safari zao.













Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527