KENYA YAREKODI IDADI KUBWA ZAIDI YA MAAMBUZI YA CORONA NDANI YA SAA 24....MAAMBUKIZI SASA YAMEFIKA 535


Waziri wa Afya  nchini Kenya Mutahi Kagwe almetangaza kwamba visa vya maambukizi ya corona  nchini humo  vimefika 535 baada ya watu 45 zaidi kupatikana na maradhi hayo. 


Kwenye hotuba yake kwa vyombo vya habari leo Jumanne, Mei 5, Kagwe amesema hii ni idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu kisa cha kwanza cha COVID-19 kuripotiwa Machi 13, 2020. 

Kati ya visa hivyo 45, 30 ni wanaume na 15 ni wanawake. Mutahi amesema kwamba watu 29 ni wakaazi wa Nairobi, 11 kutoka Mombasa na watano kutoka Wajir.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post