TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA


Tarehe 14.04.2020 majira ya 06:30hrs huko eneo la gereza kuu butimba watuhumiwa Yusuph s/o Benard, miaka 34, mnyamwezi mahabusu no 3444/2016 na Seleman s/o Seif, miaka 28, muha, mahabusu no 1177/2017 wa kesi za mauaji walijaribu kutoroka kwenye gereza hilo ndipo askari magereza wakishirikiana na wananchi waliwakimbiza na kufanikiwa kuwakamata ambapo wananchi waliwashambulia kwa kipigo katika sehemu za miili yao nakupelekea hali zao kuwa mbaya, baadae walipelekwa hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-Toure kwa ajili ya Matibabu, lakini majira ya saa 18:30hrs walifariki dunia wakati wakiendelea na matibabu.

Aidha mtuhumiwa wa tatu katika utoro huo aitwaye George s/o Aloyce, mnyambo, miaka 34, mfungwa no 200/2019 aliyekuwa amefungwa kwa kosa la uhujumu uchumi miaka 15 lakini pia akiwa na kifungo kingine cha kutoroka chini ya ulinzi miezi 6, baada ya kukamatwa katika jaribio hilo la kutoroka tena kwenye gereza hilo la butimba alihojiwa na askari polisi na akawaeleza kuwa kama wangefanikiwa wangechukua tax eneo la mabatini – nyamagana na akiwa njiani kuwapeleka polisi kuwaonesha huyo dereva tax ambaye angewasafirisha kuwapeleka eneo la katoro mkoani geita walivyoshuka kutoka kwenye gari na kuanza kutembea huku akijidai anataka kuwaonesha muhusika ghafla alianza kukimbia ndipo askari polisi waliokuanae walimwamuru kusimama huku wakipiga risasi juu lakini hakutii amri ndipo walimrushia risasi zilizomjeruhi miguuni na kufanikiwa kumkamata na kumpeleka hospitali ya Seko – toure ambapo baadae naye alifariki dunia.

Wito wa jeshi la polisi ni wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa taarifa zinazohusu wahalifu ili wahusika wakamatwe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post