CHILDBIRTH SURVIVAL INTERNATIONAL (CSI) YAZISHIKA MKONO FAMILIA DHIDI YA COVID-19


Sehmu ya unga na sabuni vilivyogawiwa nchini Uganda
Janga la Corona limezidi kuwa tishio kwa nchi nyingi barani Africa kutokana na kuzidi kuenea kwa kasi hali iliyopelekea kuharibu shughuli nyingi za kiuchumi kwa familia za Kiafrika.



Familia nyingi za Kiafrika ziko kwenye mfumo wa kutafuta riziki ya kesho leo, kwa maana ya kuwa kinachopatikana leo kitatumika kesho. Kikikosekana leo basi kesho hakutokuwa na chochote mezani.

Hii ndiyo imefanya Childbirth Survival International (CSI) kuwashika mkono baadhi ya wahanga huko nchini Uganda kwa kusaidia kaya zaidi ya 25 na kuwapatia sukari, unga, mchele, na sabuni.

Mkurugenzi wa CSI, Professa Tausi Suedi alisema wameanza na Uganda ambako wamefanya kwa awamu mbili na wanataraji kufika mpaka Tanzania ambapo CSI pia wana ofisi.

"CSI tunajitahidi kuzisaidia familia, tumeanza na Uganda na tumepanga kufanya na Tanzania, tutaanzia Ukonga",alielezea Tausi.

Madam Tausi pia elieleza kwamba achilia mbali janga la Corona, CSI pia imekuwa ikisaidia kaya mbalimbali katika masuala ya Afya ya Uzazi na Elimu rika ambapo wameweza kuwafikia zaidi ya watu 300.

Sasa akitolea ufafanuzi zaidi, Mkurugenzi wa CSI Tanzania,  Stella Masala Mpanda alisema mpango mzima ni kupata fedha za kutosha kuweza kusaidia jamii kubwa zenye uhitaji wa chakula na mahitaji mengine ya muhimu.

 "Tutaanza na familia 50 kwa kuwagawia chakula na sabuni. Mpaka sasa tumepokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo Balozi wa Heshima Zanzibar ndugu Abdulsamadi Abdulrahim, Camel Oil Tanzania na washirika wengine",alifafanua Mpanda.

"Lengo letu ni kusaidia jamii kubwa zaidi hivyo tunaomba kwa yeyote mwenye kuguswa kuungana kuwakirimu wenye uhitaji, aje tuungane wote kuwasaidia wapate mahitaji ya msingi. Wanaweza kuwasilisha michango yao kwa njia ya simu 0754 432 584 kwa maana uHaba na Haba Hujaza Kibaba", alihitimisha Mpanda.

Kusoma na kufahamu zaidi kuhusu CSI, tutembelee <<HAPA>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527