TLP KUMTEUA RAIS MAGUFULI KUWA MGOMBEA WAO WA URAIS 2020


Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema kuwa Mkutano mkuu wa chama hicho  utakaofanyika Mei 9 mwaka huu hautapitisha mgombea yeyote wa Urais kupitia chama hicho na badala yake kitampitisha Mgombea wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama hicho Agustino Latonga Mrema amesema kuwa jina Mgombea Urais lilishapitishwa na Halmashauri Kuu Chama na kilichobaki ni kudhibitisha jina la Mgombea huyo.

Amesema kuwa katika uchaguzi mkuu hakuna haja ya kuweka Mgombea wa Urais kutokana na Rais aliyopo kukidhi mahitaji ya watanzania.

Amesema vyama vingine vijifunze toka kwa  Rais Magufuli namna Tanzania ilivyopata Maendeleo kwa kipindi kifupi ikiwamo kukomesha Rushwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527