AJALI YAUA WATU WATANO KWENYE DARAJA LA MCHEPUKO KIYEGEYA MOROGORO



Watu watano wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa, kufuatia ajali ya barabarani baada ya Lori kubwa la mizigo, kuigonga gari ndogo ya abiria aina ya Noah, wakati likisubiri kuvuka katika daraja la mchepuko la kiyegeya, ambalo lilisombwa na maji mwanzoni mwa mwezi Machi.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Machi 23, 2020, huku chanzo kikielezwa kuwa ni kufeli kwa breki ya Lori na kupelekea vifo vya watu wanne papo hapo na mmoja kufariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini.

Inaelezwa kuwa ajali hiyo baada ya Lori la mizigo kuligonga gari dogo aina ya Toyota Noah wakati likisubiri kuvuka katika Daraja la mchepuo la Kiyegeya,Morogoro na magari yote yakatumbukia kwenye shimo ambako ujenzi unaendelea. 

Akizungumza katika eneo la tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa, ameeleza kuwa gari hiyo ndogo ilikuwa imebeba abiria kutoka Dumila kuelekea Gairo na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta dereva wa Lori kwani alikimbia. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527