MTUME MWAMPOSA AAGA WAUMINI WAKE KUTII WITO WA JESHI LA POLISI MOSHI

 Kiongozi wa kanisa la Inuka Uangaze, Nabii na mtume Boniface Mwamposa amelazimika kusitisha ibada kwa ajili ya kuitikia wito wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Tanzania kulikotokea vifo vya waamini wake.

Mwamposa ambaye huendesha ibada zake katika eneo la Tanganyika Packers, leo Jumapili Februari 2, 2020, amelazimika kufupisha ibada ya kwanza na kuanza safari ya kuelekea Moshi alikoitwa na polisi.

Kawaida ibada hiyo huisha kati ya saa saba hadi saa nane mchana, lakini leo imeisha saa 4:30.

Mwamposa akiwa ameambatana na wasaidizi wake, aliondoka katika eneo hilo la Kanisa 4:30 leo asubuhi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post