Picha : WANAFUNZI 700 WA SHULE YA SEKONDARI SHINYANGA 'SHY BUSH' WAANDAMANA ZAIDI YA MASAA MANNE KWENDA KWA MKUU WA MKOA

Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Wanafunzi zaidi ya 700 wa shule ya Sekondari Shinyanga maarufu 'ShyBush'  wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wameandamana hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, umbali wa zaidi ya kilomita 30 kufikisha kilio chao wakidai kunyanyaswa na mkuu wao wa shule Malambi Malelemba na mwalimu wa nidhamu  Rajabu Khamisi.

Wanafunzi hao wameanza kuandamana leo Ijumaa Februari 14,2020 kuanzia majira ya 11 alfajiri hadi saa tatu asubuhi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack huku wakiamini kuwa yeye ndiye anayeweza kutatua tatizo lao kutokana na kuvumilia kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi wa kusikilizwa.

Kaka mkuu wa shule hiyo Mwendesha Manyangu akizungumza kwa niaba ya wanafunzi amesema malalamiko mengi ya wanafunzi ya kudai kutotendewa haki na mkuu wao wa shule Malambi Malelemba pamoja na baadhi ya walimu akiwemo wa nidhamu yameshindwa kupatiwa ufumbuzi ndiyo maana wameamua kwenda kwa mkuu wa mkoa ili kupata ufumbuzi.

Kiongozi huyo wa wanafunzi alisema wanafunzi wanashindwa kujua simu wanazokamatwa nazo zinakwenda wapi kwani hawazioni zikichomwa moto licha ya kujua kuwa hairuhusiwi kuwa na simu pamoja na kupewa adhabu kwa makosa ambayo wangeweza kuonywa na baada ya kubaini hayo walikubaliana kwenda kwa mkuu wa mkoa kufikisha kilio chao.

“Tunaamini mkuu wa mkoa atatusikiliza  na kutatua matatizo yaliyopo na hapa tatizo ni mkuu wetu wa shule tunapomueleza matatizo yaliyopo hayapatii ufumbuzi hata idara ya nidhamu nao hawachukui hatua sasa mwanafunzi anaambiwa anyoe kipara wakati haitakiwi, anapewa adhabu”,alisema Manyangu.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amewasihi wanafunzi hao kuacha kujiingiza kwenye migomo isiyo ya maana ambayo inawapotezea muda wa masomo yao,huku akiwataka kuzingatia maadili na kujiepusha na vitendo ambavyo vitarudisha nyuma maendeleo ya taaluma yao na kushindwa kufikia ndoto zao.

Aliwataka wanafunzi kuwa watulivu kwani suala lao analifanyia kazi ili kuhakikisha changamoto zilizopo zinatatuliwa,huku akiiagiza idara ya elimu halmashauri ya Kishapu kuhakikisha wanafika shuleni hapo na kutatua changamoto za wanafunzi ikiwa ni pamoja kufuatilia maendeleo yao.

Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Joseph Paul aliwataka wanafunzi kuachana na makundi ambayo hayawajengi kuanzisha migomo isiyo na maana na kuwaeleza kuwa anawashukuru kwa kuwa hawakufanya fujo na kuharibu mali za shule.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shinyanga wakiingia kwenye geti la kuingia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya kuanza maandamano yao majira ya saa 11 alfajiri. Picha na wapiga picha wa Malunde 1 blog


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shinyanga wakiingia kwenye geti la kuingia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya kuanza maandamano yao majira ya saa 11 alfajiri.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shinyanga wakiwa wamekaa chini wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shinyanga wakipanda kwenye gari la polisi kwa ajili ya kurudishwa shuleni kwao baada ya kukutana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shinyanga wakipanda kwenye gari la polisi kwa ajili ya kurudishwa shuleni kwao baada ya kukutana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack

Wanafunzi wakiwa katika eneo la Ibadakuli barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Wanafunzi wakiwa katika eneo la Ibadakuli barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Wanafunzi wakiwa katika  barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

Wanafunzi wakiwa katika  barabara ya Shinyanga - Mwanza wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

Picha na wapiga picha wa Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527