MALAWI YAHALALISHA MATUMIZI YA BANGI

Nchini Malawi bangi itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Malawi imekua nchi ya hivi karibuni iliyoko Kusini mwa Afrika kuhalalisha kisheria ukulima na uuzaji wa ndani na nje wa bangi.

Wanaotumia bangi kama kiburudisho wanaiona bangi kama , "Malawi Gold", yaani Thahabu ya Malawi kama wanavyoiita wenyewe, kuwa moja ya dawa nzuri.

Lakini maafisa wamezuwia matumizi ya kisheria ya bangi kwa mtu binafsi.

Itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Mauzo ya bangi yanaweza kuchukua nafasi ya biashara ya tumbaku, ambayo inategemewa sana na Malawi.

Nchi nyingine za Afrika zilizolegeza sheria juu ya ukulima wa mmea wa bangi ni pamoja na Afrika Kusini, Zambia, Lesotho na Zimbabwe

Nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa.

Lesotho

Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo. Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.Image captionMaeneo ya nyanda zaa juu ya Lesotho yana udongo wenye rutuba unaofaa kwa kilimo cha bangi

Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini

Nchini Afrika Kusini Mahakama ya kikatiba nchini Afrika kusini ilihalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha mwaka 2018.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kuima kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi walisheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''. Hata hivyo ni haramu kutumia bangi katika maeneo ya Umma au kuiuza.Image captionMampho Thulo huvuna bangi bila kibali

Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini lilifurahia uhalalishwaji wa matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.

Ghana

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .

kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.

pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.
Korea Kaskazini

Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.
CHANZO- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم