RC TELACK AWASHUKIA WATUMISHI WALIOKAIDI KUHAMIA USHETU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akikagua daftari la mahudhurio ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu wakati wa ziara yake jana tarehe 30/01/2020

***
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ambao hawajahamia makao makuu ya Halmashauri, kata ya Nyamilangano, wahamie mara moja vinginevyo watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Telack ametoa agizo hilo jana tarehe 30/01/2020 katika ziara yake kwenye Halmashauri hiyo, kwa lengo la kukagua usimamizi na uendeshaji wa miundombinu ya shule.
Akiwa kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri, Mhe. Telack amekagua daftari la mahudhurio na kubaini kuna utoro na uchelewaji mkubwa wa Watumishi kutokana na baadhi yao kuishi Kahama mjini.

"Watumishi wote ambao hawajahamia Ushetu nipate orodha yao kwa majina na kuanzia leo naanza kuwachukulia hatua" amesema Telack.

Aidha, Mhe. Telack amewataka Wakuu wa shule zote Mkoani hapa kusimamia ufundishaji na mahudhurio ya wanafunzi ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mitihani ya mwisho.

"Hatutaweza kufanya vizuri kwenye taaluma kama Wakuu wa shule hamsimamii ufundishaji"

Naye Katibu Tawala Mkoa bw. Albert Msovela amewataka watumishi wote kusimama kwenye nafasi zao na kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post