WALIOVUNJA BAR NA KUIBA K VANT WAFIKISHWA MAHAKAMANI KAHAMA

Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog Kahama 

Wakazi wawili wa Mtaa wa Malunga wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Meshaki Joakimu (31) na Godfrey Luka (32) wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kahama kwa tuhuma ya kuvunja baa(grocery) na kuiba fedha, na thamani mbalimbali za ndani pamoja na vinjwaji  Mali ya Eliasi Mwasenga.

Akisoma Shauri hilo Januari 14 mwaka huu mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Felix Mbisse mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidi wa Mahakama hiyo Evodia Kyaruzi amedai watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Oktoba 8 mwaka 2019 usiku majira ya saa nane usiku.

Alisema kuwa baada ya kuvunja baa hiyo waliiba Televisheni mbili,bia kreti 5,konyagi chupa 10,K vant chupa 10,flash disck mmoja vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya shilingi milioni mmoja laki sita na elfu ishirini mali ya Eliasi Mwasenga.

Katika shauri hilo la jinai namba 10 la mwaka huu Mbisse alisema kuwa wawili hao kwa pamoja wanatuhumiwa kutenda makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni la kuvunja nyumba kinyume na kifungu 296 cha kanuni ya adhabu sura 16 marejeo ya mwaka 2002.

Shitaka la pili wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuiba mali hizo kinyume na kifungu cha 258 (1) na 265 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

Washitakiwa wote kwa pamoja walikana kutenda makosa hayo na Shauri hilo limeahirishwa hadi Januari 24 mwaka huu na wameachiliwa huru kwa dhamana baada ya kutimiza mashariti yake ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini wawili wawili ambao walisaini bondi ya shilingi milioni mmmoja kila mmoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527