UMEME UKEREWE BEI JUU, UNIT MOJA INAUZWA TSHS 2500 BADALA YA TSHS 100


Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dk Medard Kalemani ametoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kuhakikisha anafuatilia gharama za umeme zinazotozwa kwa wananchi wa kisiwa cha Ukerewe mkoani humo.


Imeelezwa leo bungeni kuwa Watumiaji wa umeme katika Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza wanatumia nishati hiyo kwa gharama ya Sh2,500  kwa uniti moja badala ya Sh100 inayotozwa kwa maeneo mengine.


Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma leo  na Mbunge wa Ukerewe (CCM), Joseph Mkundi wakati akiuliza swali la nyongeza akiitaka Serikali  kuchukua hatua.

Akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema jambo hilo halikubariki.

Dk Kalemani amesema Mtanzania yeyote anayetumia umeme usiozidi uniti 70 kwa mwezi, anapaswa kulipia kiwango cha Sh100 kwa uniti siyo gharama ya huko.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527