NAIBU WAZIRI WA AFYA DR NDUGULILE ATUMBUA WAWILI HOSPITALI YA TUKUYU


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ameagiza kuwekwa ndani na kutolewa katika nafasi zao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tukuyu Bw, Manase Ngogo  na Afisa Ugavi Bi. Vumilia Mwaijande kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wao.

Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo Wilayni Rungwe mkoani Mbeya wakati alipotembelea Hospitali ya Tukuyu na kujionea utendaji mbovu wa Hospitali hiyo katika kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt.Ndugulile amegiza kukatwa na kuwekwa ndani kwa Mfamasia na Afisa Manunuzi wa Hospitali hiyo kutokana na usimamizi mbovu wa stoo ya dawa na kukosekana kwa taarifa sahihi za Dawa zinazotoka na zinazoingia katika stoo hiyo.

“Nilishapata taarifa za wizi wa dawa Tukuyu sasa hili linadhibitisha hilo, huwezi ukamuweka Afisa Ugavi asimamie stoo ya Dawa wakati Mfamasi yupo” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha Dkt. Ndugulile amesikitishwa na utendaji mbovu wa Hospitali hiyo usiozingatia maelekezo ya Wizara katika uendeshaji wa Hospitali katika maeneo tofauti ya utoaji huduma.

Dkt. Nduguile amewapa onyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, muuguzu Mkuu wa Wilya na Mfamasia wa Hospitali na kuwataaharalisha na utendaji wao wa akzi kwani umekuwa sio wa kuridhishwa na ameahidi kuwangalia kwa karibu zaidi.

“Katika ziara zangu zote sijawahi kuona utumbo kama huu niseme tu sijaridhishwa na utendaji wenu kabisa na Mganga Mkuu wa Mkoa chukua hatua Wilaya ya Rungwe hatufanyi vizuri katika Sekta ya Afya tunamuangusha Mhe.Rais Magufuli” alisema Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Rungwe Mnkondo Bendera amesema kuwa kama Wilaya hawezi kuvumilia uozo wa watoa huduma za afya kwani wataendelea kuangalia kwa karibu Sekta ya afya na watakaogundulika wanahujumu Sekta hiyo watachukuliwa hatua kali.

“Kwakweli hatuvumiliahaya kama ninyi wasaidizi wetu katika Sektaya Afya mnambinu za kutuhujumu katika jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa huduma bora za Afya kwa wananchi basi tutawashughulikia ipasavyo” alisema Bw. Bendera.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527