Picha : RAIS MAGUFULI ASAJILI LAINI YA SIMU...AONGEZA MUDA WA USAJILI HADI JANUARI 20,2020


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho chake cha Taifa Msajili wa laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin aliokwenda kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019,ambapo ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2020 ndiyo utakuwa mwisho wa zoezi hilo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka alama ya kidole gumba alipokwenda kusajili Laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole katika  kampuni ya simu ya Airtel Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.Kushoto ni Msajili wa laini za Simu wa Airtel tawi la Chato Michael Martin.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Msajili wa laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin baada ya kusajili Laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita Desemba 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha simu yake ambayo ametoka kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kisha kuzungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote ambapo ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2020 ndiyo utakuwa mwisho wa zoezi hilo. 
Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita Desemba 27,2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2020 ndiyo utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mjasiliamali wa Chipsi  Joseph Wandwi wa Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2020ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mjasiliamali wa Chipsi  Joseph Wandwi wa Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2020 ndiyo utakuwa mwisho wa zoezi hilo.

Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Desemba, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole na kuwasisitiza Watanzania wote wahakikishe laini zao za simu zinasajiliwa kwa alamu za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Rais Magufuli amefanya usajili huo Chato Mjini katika Mkoa wa Geita. Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli ameongeza siku 20 kuanzia tarehe 01 Januari, 2020 hadi tarehe 20 Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA kutokana sababu mbalimbali zikiwemo kuugua na kukamilisha upataji wa namba ama Vitambulisho vya Taifa.

Mhe. Rais Magufuli amesisitiza kuwa baada ya muda huo hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa.

Amefafanua kuwa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi ikiwemo kuepusha vitendo vya utapeli na ujambazi vinavyofanywa na wahalifu, ambao licha ya wengi wao kukamatwa na vyombo vya dola wameendelea kusababisha usumbufu na upotevu mali za wananchi hususani fedha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527