UANDIKISHWAJI WATOTO SHULE ZA AWALI NA MSINGI WAONGEZEKA TANZANIA

Image result for twaweza
Na Hellen Kwavava Dar es Salaam.
Uandikishwaji wa watoto kwa Shule za Awali na Msingi nchini umeongezeka kutoka asilimia 35 kwa mwaka  2015 hadi kufikia asilimia 78 kwa mwaka 2017 na hiyo imetokana na kupatikana kwa elimu bure ambayo ni sera ya serikali ya awamu ya tano toka ilivyoingia madarakani.


Aidha shule moja kati ya nne  ndiyo inatoa chakula kwa asilimia 90  kuanzia asubui hadi Mchana na hasa kwa upande wa mjini pekee.

Akizungumza  wakati akizindua Ripoti  ya saba ya uwezo katika tathimini ya kujifunza kusoma na kufanya  hesabu Tanzania ya  mwaka 2019 Mkurugenzi wa Twaweza nchini Aidan Eyakuze alisema kuwa ripoti hiyo ilijikita kuangalia namna ya uelewa kwa watoto kuanzia miaka 6 hadi 16 katika  kusoma hasa kwa wakati huu ambao serikali imewekeza katika elimu kuanzia shule za msingi hadi sekondari.

Eyakuze alisema kuwa ripoti hiyo ilibaini kuwa ufaulu kwa upande wa hesabu na kingereza kwa watoto hao bado umekuwa mdogo sana jambo ambalo ameiomba serikali kutilia mkazo kati masomo hayo ili kuongeza chachu ya watoto hao kwa kuyapenda masomo hayo na kufaulu vizuri.

“Kwenye ripoti hii tumebaini mambo kadhaa hasa kutokana na serikali hii kuwa na  sera ya kuondoa ada kwa shule za msingi hii imepelekea uandiskishwaji wa watoto kupanda lakini pia sera ya kupeleka rukuzu moja kwa moja mashuleni bila kupitia Halmashauri hasa kwa shule hizi iliyoanza kutekelezwa mwaka 2016  hii imetoa hamasa kubwa kwa shule kuhakikisha wanafunzi wana huzulia na kuandikishwa bila shida”,alisema

Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kwa kusema kuwa kwenye utafiti wao  walibaini ushiriki wa wazazi kufuatilia maendeleo  ya watoto wao ni mdogo jambo ambalo linapelekea watoto wengi kutofuatilia masomo yao kwa ufasaha lakini pia wengi wao kutohudhuria shule ipasavyo.

“Tumebaini Asilimia 50 ya wazazi hawafuatilii maendeleo ya watoto wao mashuleni hii inarudisha nyuma juhudi za serikali jambo ambalo watoto wengi huishia njiani  masomo yao huku elimu ikiwa ni bure”,aliongeza.

Kwa Upande wake Meneja  Uwezo Zaida Mgalla alisema kuwa utafiti huo waliufanya kwa wilaya 56  lakini waliona kuwa ufaulu umeongezeka kwa watoto wa darasa la tatu hasa kwenye somo la Kiswahili  toka asilimia 29 kwa mwaka 2011 hadi kufikia 62 kwa mwaka 2017 ambapo kwa darasa la saba wengi wanamaliza wakiwa hawajui kusoma Kiswahili na kingereza.

“Utafiti huu tumeweza kufanya pia kwa vijiji 1680 na tuliweza kuhusisha wadau mbalimbali katika kufanya utafiti huo lakini tulibaini kuwa bado tuna idadi ya asilimia 64 ya watoto wanaomaliza darasa la saba bila kujua kusoma kwa ufasaha kingereza”,alisema Zaida.

Bi Mgalla alisema kuwa Utafiti huo walifanya kwa kutumia mtaala wa Serikali wa Darasa la pili hivyo ulitoa urahisi kwa watoto hao kuelewa maswali walioweza kuulizwa na wao kufanyia tathimini.

“Tulishirikiana  Baraza la mtihani la Taifa kuweza kutumia mtaala wao ili kupata takwimu zilizo bora  na zenye uwakika”,aliongeza.


Hata hivyo Utafiti huo ulifanyika kwa makundi Matatu ambapo ni watoto wenye Umri wa Miaka 9 hadi 13 waliopo shuleni na nje ya shule,Watoto wanaosoma shule walio darasa la tatu hadi saba na watoto ambao hawasomi shule kabisa wenye umri wa Miaka 9 hadi 13.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527