MWIMBAJI WA INJILI AMUUA MKEWE KWA KUMKATA SHOKA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha nchini Tanzania linamtafuta Moses Pallangyo akidaiwa kumuua kwa kumkata shoka mkewe Marry Richard Mushi mkazi wa kijiji cha Kilinga wilayani Arumeru mkoani humo.


Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Jonathan Shana amesema tukio hilo limetokea leo Jumatano Desemba 25, 2019 mchana kutokana na ugomvi wa kifamilia.

"Baada ya kufanya mauaji ametoroka na tunamsaka lakini chanzo kamili cha ugomvi hakijulikani lakini taarifa za awali zinaeleza huenda ni wivu wa mapenzi," amesema Shana

Pallangyo ambaye ni maarufu kwa jina la Moses Lebaba ni mwimbaji wa kwaya za Kiinjili mkoani Arusha.

Baba wa mtuhumiwa, Latiaeli Pallangyo anasema tukio hili limetoka ikiwa ni wiki tatu tangu marehemu aanze kuishi na mwanae kama mke na mume.

"Hapakuwapo na ugomvi wowote na walitegemea kusherehekea sikukuu ya Krisimasi vizuri. Mara baada ya Marry kupika chai aliendelea na shughuli za kawaida mpaka mauti yalipomfika kwa kupigwa na shoka chumbani kwake," amesema
Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527