COSTECH YAJA NA UBUNIFU WA KIFAA CHA KUONGEZA JOTO KWA WATOTO NJITI CHA BEI RAHISI


Mkurugenzi wa Tantrade Bwana Erick Rutageruka akiwa na Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Stella Manyanya kwenye banda la Costech
Mbunifu wa Kifaa  cha kuhifadha Joto watoto wachanga (INCUBATOR) Daktari Emanuel Mushi Akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Stella Manyanya namna ya kifaa kilivyo kwa ndani.
Daktari Mushi akifungua Incubator ya Joto mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda  Stella Manyanya.


 Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Daktari Mbunifu Emanuel Mushi wamebuni mashine ya kuhifadhia joto watoto wanaozaliwa wakiwa wamechoka na ambao hawajatimiza wakati ili kuokoa maisha yao

Akizungumza  kwenye Viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba katika maonyesho ya nne ya bidhaa za Viwanda vya Tanzania Mbunifu wa Kifaa hicho, Dkt. Emanuel Mushi amesema kuwa kifaa hicho alikifanyia majaribio kwa muda wa miaka 6 na amekipa jina la (EMBRANES WOMB) kina uwezo wa kutunza joto la mtoto la kutosha na kinafanya kazi vizuri.

“Nilipoona tatizo la watoto njiti ni kubwa nikaona kuja na ubunifu wa mashine hii kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto hasa upande wa vijijini ambao wanasafirishwa kutoka hospitali ya kijiji hadi hospitali ya mkoa ili kupata matibabu zaidi ya kiafya hivyo na joto la mtoto linaweze kuwepo na kufanya damu itembee kwa urahisi mwilini”,amesema

Ameongeza kuwa kifaa hicho kina uwezo sawa na mashine ya kawaida ya kuongezea joto watoto kilichopo katkika zahanati mbalimbali ambapo ameitaka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto kumtumia kwa ufasaha katika kuzalisha mashine nyingi zaidi na kuzisambaza katika vituo vya afya ambayo hutoa huduma ya mama na mtoto kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto wengi zaidi ili kujenga taifa lenye watoto wengi na uchumi imara.

“Mashine hii nimeibuni mimi mwenyewe kwa taaluma yangu ya Udaktari lengo langu ni kuokoa mamilioni ya watoto kwa kutengeneza vifaa vya kuwaongezea joto watoto pamoja na vifaa vya kuhifadhi joto kwa ajili ya kumsafirishia mtoto kutoka hospitali ya ya vijijini hadi hospitali ya mkoa",amesema 

Dkt Mushi amesema kupitia ubunifu wake huo ameweza kufanikisha kujengwa kwa kituo cha afya cha mama na mtoto kilichopo katika mkoa wa Manyara ambapo wanawake wengi sasa wanafika na kujifungua katika kituo hicho.

“Kwasasa Mkoa wa Manyara umeweza kuwa na kituo cha afya cha Mama na Mtoto na hiyo ni kutokana na kuwa na kifaa kinachoweza kuokoa maisha ya Mtoto pia hasa aliye katika hali hatarishi hasa la kukosa joto na kuzaliwa wakati amechoka”,ameongeza Dkt. Mushi.

Hata hivyo ameiomba serikali kuwekeza katika vifaa hivyo ili waweze kutengeneza vifaa vingi zaidi kwajili ya kuokoa watoto wachanga wanaokosa joto baada ya kuzaliwa.

Watoto waliozaliwa kabla ya kuhitimu muhula au wakiwa na uzani wa chini wako katika hatari zaidi ya kufa kutokana na hipothemia, maambukizi, matatizo ya kupumua na kutokomaa kwa viungo muhimu na Kinachofuatia ni kuwa watoto hawa hushindwa kukabiliana na maisha nje ya uterasi na Watoto hawa wana kiwango kidogo cha mafuta ya ngozi, hasa mafuta ya rangi ya kahawia, mafuta haya ni muhimu sana katika kutolesha joto kwa mtoto mzawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post