KALEMANI: TANZANIA INA AKIBA YA GESI FUTI ZA UJAZO TRILIONI 57.54


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
SERIKALI kupitia Wizara ya nishati imesema Tanzania ina akiba ya gesi futi za ujazo trilioni 57.54 huku matumizi ya rasilimali hiyo kwa sasa ni futi za ujazo trilioni 0.5 tu.

Kutokana na hayo imesema itashirikiana kwa ukaribu zaidi na asasi za kiraia kuhakikisha wanaleta maendeleo ya uchumi wa viwanda kwa kutumia rasilimali gesi.
 
Hayo yamebainishwa    Nov.6,2019  na waziri wa nishati Medardi  Kalemani wakati akitoa taarifa ya nishati  kwenye jukwaa la tisa la wadau wa sekta ya uziduaji wa mafuta ,  gasi  na madini Katika wiki ya AZAKI inayoendelea Jijini hapa.

Waziri Kalemani amesema matarajio ya serikali  ni  kuhakikisha rasilimali hiyo inashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa viwanda na kuchochea maendeleo ya taifa na wananchi wake.

Pamoja na hayo amesema ,jitihada za Serikali zinaendelea Katika kuhundua mafuta kwa manufaa ya watanzania .

Aidha Mhe.Kaleman ame sisitiza masuala ya uwazi,uwajibikaji na ufuatiliaji wa uhakika  Katika masuala ya gesi unapaswa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia teknolojia na ubunifu kwa uchumi wa viwanda.
 
Kwa upande wake Naibu waziri wa madini  Stanslaus Nyongo akizungumza katika jukwaa hilo alisema tangu serikali kufungua masoko ya madini katika maeneo mbalimbali nchini mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa umeongezeka maradufu  huku asilimia 97% ya Watanzania mgodi wa Geita GGM wameajiriwa.

Aidha amesema ,Licha ya mafanikio hayo  vitendo vya ulanguzi kwa wachimbaji na utapeli wa watu kuuziwa madini bandia vimetoweka kabisa kutokana na umakini unayofanywa na Serikali.

Pamoja na hayo alisema ,Katika kuhakikisha ulinzi Katika sekta ya madini ,Serikali iliwakamata wanunuzi tisa wa madini ya dhahabu ambao walikiuka Sheria ya ununuzi.

Hata hivyo amebainisha kwamba,kwa Sasa Serikali kwa kushirikiana na Serikali za mitaa inatupia jicho kwa wachimbaji wadogo ili kuwawezesha ajira na kusaidia kuongeza pato la Taifa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo alisema  Serikali inapambana kuondoa vikwazo kwa wanawake Katika sekta ya madini  .

Amesema wanawake wamekuwa wakikumbana na vikwazo kwa kuchimba dhahabu  kwa kubahatisha kwa kuwa hawana taarifa sahihi za kijiolojia.

"Kupitia Shirika letu la stamiko Serikali inaendeleza huduma kwa kutoa elimu kwa wachimbaji wanawake kuhusu madini juu ya utafiti,uchenjuaji  na uzalishaji,"alisema.
 
Awali akizungumzia umuhimu wa jukwaa hilo mkurugenzi mtendaji wa Haki Rasilimali Rachel Chagonja amesema jukwaa hilo limelenga kujadili kwa pamoja ubia kati ya serikali wadau na wananchi kuhusu ushiriki kwenye sekta ya mafuta gesi na madini kwa maendeleo ya taifa na wananchi wake.

Amesema ,sekta hiyo inakabiliwa na mfumo dume kutokana na kukosekana uwiano sawa wa kijinsia huku wanawake wakinyanyasika na kudharauliwa hasa katika maeneo ya migodini na kuiomba Serikali kuwashirikisha zaidi wanawake Katika uchumi was viwanda.

Mwenyekiti wa bodi kutoka Haki Rasilimali  Bw.Donald Kasongi amesema asasi ya Haki Rasilimali inahakikisha inaboresha kipato kwa wananchi kutokana na Rasilimali zilizopo nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527