Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Ben William ameachia wimbo mwingine mpya unaitwa Imela.
Wimbo wa Imela umerekodiwa katika Studio za Apex Music zilizopo jijini Mwanza na video imeongozwa na Muongozaji King Sabe.
Wimbo huu wa pekee umenakishiwa na vionjo vya lafudhi kutoka lugha mbalimbali ambazo ukisikiliza unapata upako na kumsifu Mungu kwa neema na kipaji kikubwa cha Ben William.
Wimbo wa Imela umetoka baada ya kutoa wimbo wa Emmanuel, ambao pia unaendelea kufanya vizuri sana.
Tumia dakika zako chache kutazama video ya Imela kutoka kwa Ben William hapa chini
Social Plugin