WAZIRI UMMY AWATAKA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII KUACHA KUPOTEZA MUDA WAO KUTUMIANA KATUNI KWENYE MAKUNDI YA WHATSAPP | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 23, 2019

WAZIRI UMMY AWATAKA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII KUACHA KUPOTEZA MUDA WAO KUTUMIANA KATUNI KWENYE MAKUNDI YA WHATSAPP

  Malunde       Wednesday, October 23, 2019
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa afya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh Ummy mwalimu amewataka wataalamu wa  Maendeleo ya Jamii kuongeza kasi ya kuhamasisha jamii ili itumie teknolojia zitakazowasaidia kubadilisha maisha yao  na kupata muda zaidi wa kufanya shughuli za maendeleo.

Waziri ummy ameyasema hayo jana  jijini Dodoma wakati akifungua kongamano na mkutano mkuu wa sekta ya maendeleo ya jamii wa mwaka 2019, pamoja na  kuzindua mwongozo wa majukumu ya wataalamu wa maendeleo ya jamii na chama cha watalaamu wa maendeleo ya jamii huku pia akiwataka kuacha kutumiana katuni kwenye makundi ya Mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Whatsaap.

Aidha, Waziri ummy ameongeza kuwa ni wajibu wa wataalamu wa maendeleo ya jamii kuwafikia wanachi katika kupata    maendeleo  licha ya kuwa ziko changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili ambapo amewataka  kutokujiweka nyuma katika utendaji wao wa kazi kila siku na kuwasisitizia kuwa wabunifu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Maendeleo ya jamii kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia ,wazee na watoto Patrick Golwike amesema kongamano hilo limefanyika kwa nia ya  kuwakutanisha watunga sera na watekelezaji ili kutathmini utekelezaji wa malengo ambayo wamejipangia.

Nae Rais wa Chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii, Wambura Sunday amesema chimbuko la chama hicho ambacho waziri ummy amezindua ni chimbuko la matokeo ya mkutano mkuu wa watalaamu wa maendeleo ya jamii uliofanyika November 2017 katika ukumbi wa nyerere katika chuo cha mipango ya maendeleo vijijini, jijini hapa.

Hatahivyo, Waziri ummy amesema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa  na wataalamu  wa maendeleo ya jamii hapa nchini  kwani juhudi  zao zimekuwa na manufaa na jamii imeendelea kutambua wajibu wao wa kushiriki  katika maendeleo  .


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post